Posts

Showing posts from December, 2020

Shairi: IWAJE?

Image
IWAJE? Wewe ulitakaje? Shule za msingi Vitu vifanyikaje? Katikati ya vipindi Watoto walaje? Kwa elimu-ushindi Mimi kama wewe Nina uwezo kufikiri Nafikiri mwenyewe Siwezi shikiwa akili Mwenye haki apewe Vinginevyo ni ukatili Haki ya kuelimika Na malezi stahiki Hakizo kuzishika Mtoto huwa rafiki Mzaziye wajibika Utajaona mantiki Mapumziko wasile! Darasani waingie Njaa iwazingile Somo lisiwaingie Shule waikimbie Maoniyo niambie? Wale chakula vizuri Darasa changamfu Wasipate tena sifuri Utoro ugeuke hafifu Wawe watoto wazuri Wenye afya nadhifu. Changia mawazo Tupate mwongozo Tuwajengee uwezo Elimu bora ni nguzo Hatua hizi mwanzo Tuvishinde vikwazo #NilisheNifaulu Fasmo Tanzania Nobel was Here😊

NILISHE NIFAULU

Image
NILISHE NIFAULU Ni mradi unaotekelezwa na asasi isiyokuwa ya kiserikali ya FASMO ikishirikiana na wanajamii. Mradi huu umelenga utoaji wa chakula katika shule za msingi kama njia kuu ya kuchochea mahudhurio na utulivu wakati wa kujifunza ambavyo kwa pamoja huchangia matokeo bora (ufaulu) kwa wanafunzi na shule kwa ujumla. Familia nyingi za Kitanzania zina uwezo mdogo wa kiuchumi. Watoto hulazimika kuamka asubuhi sana na kukimbilia shule bila kupata kitu chochote cha kula. Na kwa bahati mbaya hata shuleni hakuna utaratibu wa ugawaji wa chakula hivyo mtoto hujikuta masaa zaidi ya saba hajapata chakula kwa kuwa hata hela ya matumizi shuleni hajapewa au ni ndogo sana.  Uelewa wa wanafunzi huwa hafifu kutokana na mazingira hayo ya ukosefu wa chakula wakati wa masomo. Pia ukosefu wa chakula huchochea sana utoro na wanafunzi kuacha shule.  Utoro katika sura mbili, sura ya kwanza wanafunzi kutokuja shule na sura ya pili mwanafunzi au wanafunzi kutohudhuria kipindi au vi...