MAISHA YETU YA KILA SIKU NA UCHANGIA WA DAMU.
Juni 14 ni siku ya kuadhimisha kuchangia damu duniani. Siku hii hutumika kuwashukuru watu wote wanaojitolea kuchangia damu na kuhamasisha wengine ili waweze kuanza kuchangia damu. Damu hutumika kusaidia kuokoa maisha ya watu wengi sana duniani kama vile, watu waliopata ajali, wanawake wanaojifungua na watu wenye magonjwa mbalimbali kama vile upungufu wa damu mwilini (anemia). Kuchangia damu ni kitendo cha mtu kutoa damu yake ambapo huhifadhiwa katika mfuko maalum (blood bag) na kuwekwa katika joto kati ya nyuzi joto (°c) +2 hadi +6. Joto hilo ni sahihi katika kuhakikisha vitu vilivyomo ndani ya damu kama vile seli nyekundu, chembe sahani na vinginevyo haviharibiwi na damu haishambuliwi na vijidudu hatari kama vile bakteria na virusi. Tujikumbushe vitu vichache kuhusu damu na kuchangia damu Damu ni moja kati ya tishu katika miili ya wanyama (binadamu) ambayo hutumika kusafirisha virutubishi, takamwili, oksijeni, homoni na vitu vingine mwilini..Uwepo wa seli nyekundu za damu