Posts

Showing posts from August 20, 2020

Mradi wa MSINGI WA LISHE BORA katika Manispaa ya MOROGORO MJINI

Image
MSINGI  WA LISHE BORA Msingi wa lishe bora ni mradi wa utoaji elimu ya lishe kwenye shule za msingi katika manispaa ya Morogoro mjini. Mradi huu umelenga kuwajengea watoto tabia na maarifa ya kujua masuala ya msingi ya lishe yatakayowasaidia kufanya maamuzi sahihi katika ulaji bora na ulaji wa afya ili kuwaepuka kupata magonjwa na matatizo ya kiafya yanayohususiana na lishe kama kisukari, matatizo ya mifupa, matatizo ya moyo, matatizo ya ini na unene uliokithiri.. Maarifa hayo ni pamoja na kujua namna nzuri za kupangilia mlo kamili kwa kujumuisha makundi yote ya chakula, kuwajengea tabia ya usafi wa chakula na mwili, kuwafumbua akili juu ya vyakula vipi wasivipe kipaumbele kwenye milo yao kutokana na wingi wa vyakula hivyo hugeuka hatari kwenye afya zetu.  Pamoja na hayo pia elimu juu ya vitu mbalimbali vya afya kama kuwafundisha ustaarabu wa mezani (table manners), mitindo mizuri ya kukaa ili kulinda afya ya mifupa na nyama pamoja na umuhimu wa Bima ya afya. Morogoro mjini