Posts

Showing posts from April 18, 2020

KUKATAA MAARIFA NI UJINGA ULIOKOMAA

Image
Naomba nianze kwa kucheka kidogo (haha ) kuna kauli nyingi sana zinazoumiza ukizisikia mtu akisema ila zinachekesha ukizitafakari. Bila shaka umewahi sikia kauli "Sikiliza wewe sisi ndio wataalamu....". Hiyo kauli ni moja ya kauli maarufu tu kwenye mitandao ya kijamii hapa nchini kwetu Tanzania. Nje ya hio kauli kuna kauli zingine kama.. ●Utaniambia nini wewe? ●We mtoto wa juzi unajua nini? ●We wakuja utatueleza nini sisi wazawa? ●Mkubwa hakosei ●Nimeanza kuliona jua kabla yako huna chakuniambia sikijui ●Kwani yenye elimu mkubwa wamenipita nini mimi?   Siwezi zitaja kauli zote kwakuwa ni nyingi na kila siku zinakuja kwa mfumo tofauti ila zote zinakuwa zimejengeka katika kukataa maarifa mapya au maarifa mbadala kutoka kwenye taasis za kutoa elimu au kutoka kwa watu waliotuzunguka.   Tangu kuumbwa kwa dunia mpaka leo hii nje ya mapungufu au kasoro zingine za kila mwanadamu, binadamu hajatimia kimaarifa. Kuna maarifa kila mwanadamu anakuwa na uhaba nayo au h...