UNYONYESHAJI NA FAIDA ZAKE
UNYONYESHAJI Wiki ya unyonyeshaji duniani ni kampeni ya dunia nzima inayoadhimishwa na nchi mbalimbali kila mwaka katika wiki ya kwanza ya mwezi wa nane (tarehe 1 hadi 7 mwezi wa nane) inayolenga kuhamasisha unyonyeshaji sahihi wa maziwa ya mama ili kuimarisha afya za Watoto. Katika mwaka 1992 ndipo wiki ya kwanza ya unyonyeshaji duniani iliadhimishwa. Kama ilivyokuwa miaka ya nyuma wiki ya kwanza ya mwezi wa nane (Agosti) kuadhimisha kwa wiki ya unyonyeshaji duniani, kauli mbiu ya mwaka huu ilikuwa“ Tuwawezeshe Wanawake Kunyonyesha Watoto kwa Afya Bora na Ulinzi wa Mazingira” . lengo likiwa ni kuwasaidia wazazi na wahudumu wa nyumbani kutoa huduma inayostahili kwa watoto tangu mama akiwa mjamzito, anapojifungua na hata baada ya kujifungua. Katika kuambatana na kauli mbinu ya mwaka huu, shirika la Afya duniani (WHO) na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto (UNICEF) wamelenga katika kushauri na kuziita serikali kuhakikisha zinalinda na kuchangia up...