Siku Ya Hedhi Salama
Tarehe 28 mwezi mei kila mwaka ni siku ya kuazimisha siku ya hedhi salama duniani (safe menstrual day) Kwa kifupi tujikumbushe mambo machache kuhusu hedhi Hedhi ni kipindi ambacho wanawake waliokwisha balehe hupitia ambapo huambatana na kutokwa na damu, na kwa kawaida huwa mara moja kwa mwezi..Na hii hutokea kwa sababu mji wa mimba (yuterasi-uterus) unakuwa umeandaliwa tayari kwa kupokea na kulea mimba, maandalizi haya huusisha kuongezeka kwa unene wa misuli ya yuterasi na mishipa ya damu. Pale ambapo mwanamke asiposhika mimba, ukuta wa mji wa mimba huachia au kudondoka (shading of uterus wall) na hii ndio hupelekea kutokwa na damu katika kipindi hiki ambacho kwa kawaida huchukua takribani siku 3 hadi 8, ingawa inaweza kutokea mwanamke kupata hedhi kwa muda zaidi ya siku nane kutokana na sababu mbalimbali. Kwa wanawake wengi hedhi hutokea kwa namna ambayo wao huijua na wanaweza kujua ni siku gani katika mwezi huziona siku zao ( kwenda mwezini kama inavofaha...