MADHARA YA UTENGANO WA KIJAMII YALIYOSABABISHWA NA COVID19
Madhara ya Utengano wa Kijamii yaliyoletwa na COVID19 Nchi nyingi sasa duniani zimeanza kulegeza masharti ya tahadhari zilizowekwa zifuatwe ili kupunguza na hata kutokomeza maambukizi na madhara ya janga la virusi vya Korona. Ugonjwa wa Korona umeleta madhara mengi ya muda mfupi na mengine ya muda mrefu. Itachukuwa muda jamii yetu kurudi kwenye maisha ya kawaida, kiuchumi na kimahusiano baina ya watu hili ni kutokana na tahadhari tunazochukua na tulizochukua katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Covid19. Leo naomba tuzungumzie madhara ya muda mfupi na muda mrefu ya Kujitenga kijamii (Social distancing/Isolation ). Kujitenga kijamii ni moja ya njia iliyobuniwa na kuhamasishwa itumike katika kuzuia maambukizi ya Corona. Njia hii ililenga mtu kukaa umbali wa Mita moja na zaidi na hata kujifungia ikiaminika umbali huo mtu aongeapo au akikohoa virusi haviwezi kumfikia mwingine kwenye huo umbali. Njia hii imekuwa na msaada kwa kupunguza kasi ya maambukizi ndani ya wanajamii kwenye...