Msimu wa Baridi na Afya.
Kipindi cha mwezi wa sita na mwezi wa saba maeneo mengi sana ya hapa kwetu Tanzania huwa katika msimu wa baridi kali. Kuna sehemu zingine baridi huwa kali kiasi cha saruji/barafu huwepo juu ya ardhi. Baridi hufanya sisi binadamu kuwa na tabia fulani ili tupate joto na kuishi kwa amani kipindi hiki. Tunabadili mavazi kutoka mepesi kwenda mazito, mabadiliko ya muda wa kulala na muda wa kuamka. Wengine kiwango cha usafi hupungua, kutokana usafi unategemea maji kwa sana na hayo maji kipindi hiki huwa ya baridi kiasi huogopwa. Kuna kundi la watu wao kipindi cha baridi hujikuta wanaanza kunywa pombe kali ili kuupa mwili joto bila kujali madhara ya muda mfupi na mrefu. Juu ya yote kuna tabia moja kipindi hiki cha baridi ambayo sio mbaya lakini ikikosa umakini sio salama. Tabia ya kuota moto. Moto huupasha mwili joto, wapo wanaoota kwa makundi na waoota pekeyao. Unaweza ukawa moto wa kuni au mkaa. Uotaji wa moto sio njia mbaya katika kuweka mazingira ya ujoto. Ukosefu wa umakini na kutokujua ...