MAJI NA AFYA ZETU
Maji ni afya, maji ni kinga. Kuna faida lukuki kwa unywaji wa maji. Je wajua sehemu kubwa ya mwili wa binadamu imetengenezwa kwa maji, kwa maana kwamba viungo na tishu mbalimbali mwilini vimeundwa kuhusisha maji..kwa mfano damu, misuli na hata mafuta mwilini yana maji kwa kiasi chake pia. Karibu asilimia 60 hadi 75 uzito wa mwili wa binadamu ni maji ingawa kunakuwa na tofauti za kiasi cha maji kulingana na jinsia, umri, mazingira, aina za shughuli mtu anafanya nakadhalika Dalili zinazoonesha mtu kapungukiwa maji mwilini 1. Harufu mbaya ya kinywa 2. Ngozi kuwa kavu 3. Maumivu ya kichwa (ingawa sio kila maumivu ya kichwa ni upungufu wa maji) 4. Kizunguzungu (ingawa sio kila hisia za kizunguzungu husababishwa na upungufu wa maji mwilini) 5. Uchovu wa mwili 6. Midomo kuwa mikavu (watu wengi huonesha dalili hii na huonekana sehemu ya nje ya midomo - lips) 7. Kutopata choo mara kwa mara au kupata choo kigumu na kwa shida (constipation) Kuna baadhi ya dalili hapo juu