Wanajamii Wanahitaji Elimu
Jamii yetu bado inachangamoto nyingi sana. Na kwa bahati mbaya zipo changamoto ambazo zinahatarisha ubora wa kizazi kijacho kiafya na kimaadili. Jambo zuri ni kwamba wanajamii wanazijua changamoto hizo japo sio kwa upana mkubwa. Kwa mfano wanajamii wengi wanajua lishe isipokuwa nzuri inaathiri afya lakini hawajui lishe mbovu ikoje na lishe bora ikoje. Wao miaka nenda miaka rudi watajilia kile kilichopo au kile wanachopenda. Haya twende kwenye malezi, huko nako changamoto chungu nzima. Wazazi na walezi wanajua malezi yasipokuwa mazuri yanaathiri moja kwa moja ukuaji, afya, tabia na hata masomo ya mtoto. Lakini malezi bora yamebaki kuwa changamoto kwe wengi. Usimamizi mdogo wa wazazi, mawasiliano madogo/mabaya baina ya watoto na wazazi, vipigo vikubwa, matusi na matendo mbalimbali yanayowanyima watoto haki zao za msingi. Hatari iliyopo, matendo hayo mengi yamekuwa ndiyo mtindo wetu wa kawaida wa maisha hii inapelekea wazazi kutoambilika. Majirani nao kuchukulia kawaida au kuogopa kurip...