HAKI ZA AFYA YA UZAZI NA JINSIA
HAKI ZA BINADAMU Haki za binadamu ni haki zinazohusiana na mambo ya msingi na asili ya uhuru na heshima ya ubinadamu ambapo watu wote wamepewa haki ya kupata heshima kama binadamu. Mara mtu azaliwapo mume au mke hupata haki hizi. Haki hizi zinatambuliwa kimataifa na zina usawa kwa watu wote. Nchi mbalimbali zimetia sahini na kuidhinisha haki hizi za kimataifa na kufanya ni sehemu ya sheria zao pamoja na kuweka sera zinazolinda haki hizi. HAKI ZA UZAZI Haki za uzazi ni haki zinazomwezesha mwanamke na mwanaume, mwajiriwa kutimiza majukumu yake ya uzazi na kufanya kazi bila kubaguliwa, kubugudhiwa au kupoteza ajira. Likizo ya uzazi ikiwa ni moja ya haki za uzazi, humpa mama na baba muda kutoa matunzo muhimu kwa mtoto katika siku/miezi ya mwanzo ya maisha yake, ikiwa ni pamoja na kumnyonyesha. Vilevile likizo ya uzazi humpa mama mwajiriwa muda wa kupumzika na hivyo kusaidia mwili wake kurudi katika afya na hali ya kawaida baada ya kujifungua. Haki za uzazi zina misi