SHAIRI: NJIA PANDA
NJIA PANDA Nipo njia panda, Mawazo yanizonga, Kiza kimetanda, Fikra zanigonga, Wapi pa kwenda, Kivipi nitasonga? Niache shule, Nikatumie kipaji, Niwe kama yule, Msanii mchezaji, Nivume huku kule, Kwa mdogo mtaji. Nitakuwa maarufu, Na hela kibao, Sitaishi kwa hofu, Yatakuwaje mafao, Hawatoacha kunisifu, Katika maongezi yao. Nitajenga majumba, Nakumiliki magari, Kupitia kuimba, Nitakuwa hodari, Kwa udi uvumba, Nitaiteka sayari. Shule kitu nyeti, Lakini mimi sielewi, Kwanini wenye vyeti, Nafasi hawapewi, Kwenye viti waketi, Haki hawatendewi. Shule haina manufaa, Wasomi maisha duni, Sasa wanatuhadaa, Kisiasa kuturubuni, Kutuaminisha wanafaa, Wajinufaishe kiuchumi. Kipaji changamoto, Nani wa kukusaidia, Utaishia kwenye msoto, Na kuchoka kuvumilia, Utalia kama mtoto, Ndoto zisipotimia. Elimu bado hazina, Kote ulimwenguni, Kuiacha hapana, Hata wakinirubuni, Nitakosa maana, Wataniita muhuni. Shairi la watoto..... Na Nobel Edson Sichaleh Fasmo Tanzania Childhood Develop