Ujinga ni chanzo kikuu cha ubinafsi.
Ubinafsi ni moja ya madhara ya ujinga. Mtu kuwa na hisia kali juu yake dhidi ya wengine. Kuona yeye ndio zaidi ya wengine kwenye hilo kundi, kuhisi anastahili kupata zaidi ya wengine mfano gawio la kitu chochote, kipato hata shukurani. Ubinafsi unaletwa na upofu wa uhalisia unaotokana na kutokujua uhalisia wa vitu au maisha na kujikuta unajiona au unajifikiria wewe tu Ubinafsi ni ujinga. Kutokujua pia wenzako wana thamani kama wewe, ni wahitaji kama wewe, ni watafutaji kama wewe. Ubinafsi ni kutokujua kuwa ridhiki huja kwa baraka za Mungu, kwa jitihada na kwa uwekezaji lakini wewe unachojua ni unastahili zaidi yao hata kama mpo katika daraja moja au daraja la chini yao. Kutokana na ubora wako katika jambo fulani unaona HAKUNA KAMA WEWE!! Wakati kuna watu mnaosaidiana nao, wanaokupa mawazo na kukutia moyo. Au kuna watu ambao kama nao wangepewa nafasi kama wewe wangeweza kufanya kama wewe au hata zaidi. Kupuuzia michango ya watu wengine katika maf...