FAIDA ZA KUFANYA UCHUNGUZI WA KIAFYA MARA KWA MARA
Faida za kufanya uchunguzi wa kiafya mara kwa mara . Kuna kampeni nyingi zinazohamasisha watu kufanya uchunguzi wa afya zao juu ya gonjwa fulani au hata juu ya hali ya afya ya mwili wote kwa ujumla. Kampeni kubwa ni za kuhamasisha kupima Virusi Vya Ukimwi (VVU) pia kupima chanzo cha homa "Sio kila homa ni Malaria". Pamoja na hayo kuna kampeni nyingi za kuhamasisha wanawake kupima hali zao afya hususani kwenye mifumo ya uzazi (saratani ya matiti na shingo ya uzazi) Licha ya jitihada nyingi za kuhamasisha watu kupima na kujua hali zao za kiafya zinazofanywa na serikali pamoja na asasi za kiraia lakini bado muamko wa watu umekuwa mdogo. Sababu zinazofanya muamko uwe mdogo ni pamoja na hali ya uchumi, wengi kipato chao ni kidogo kiasi hata kupata milo mitatu ni mtihani. Sababu zingine ni pamoja na uelewa mdogo juu ya umuhimu wa kuchunguza afya zao, baadhi ya Bima za Afya haziruhusu uchunguzi wa kiafya kwa asiye mgonjwa. Utaratibu ni kwamba huwezi kupima magonjwa mbalimbali kam...