Posts

Showing posts from May 16, 2020

NAMNA VIRUSI VYA CORONA VINAVYOSABABISHA COVID19 HUPIMWA

Image
NAMNA VIRUSI VYA CORONA VINAVYOSABABISHA COVID19 HUPIMWA Mpaka sasa kuna vipimo (vitendanishi) vya aina kuu mbili vinavyotumika kupima covid-19 vinavyotumika sehemu nyingi duniani kutambua watu wenye maamumbikizi ya ugonjwa huu wa mlipuko uliosambaa sehemu karibu zote za dunia. Aina ya kwanza ni kile kinacho pima covid-19 kwa kuangalia uwepo wa kinasaba cha kirusi chenyewe (RNA). Kipimo hiki hujulikana kama ‘Real-time Reverse Transcription Polymerase Chain Reaction’ (RT-qPCR) au al-maarufu PCR! Hiki ndio kipimo mashuhuri na ‘standard’ kinachotumika ulimwenguni kwa sasa. Sampuli zake huchukuliwa kwa kulambisha (swab) kijiti cha pamba (cotton swab) ndani-nyuma ya pua (nasophyaryngeal swab) na/au ndani-nyuma ya mdomo (oropharyngeal swab). Aina ya pili ni ile inayopima kwa kuangalia kinga (antibody) inayozalishwa na muathirika pindi anapopata maambukizi ya kirusi cha corona. Kipimo hichi hujulikana kama ‘Immune Rapid Test, na vipo vya aina tofauti. Aina