Posts

Showing posts with the label AFYA

Shinikizo Kubwa la Damu

Image
 SHINIKIZO KUBWA LA DAMU  Utangulizi  Moyo unapopiga, husukuma damu kwenye mishipa ya damu ili isambae mwilini kote.  Shinikizo la damu ni hali ambapo msukumo huu wa damu unazidi kiwango cha kawaida na unaweza kusababisha madhara mwilini.  Madhara ya shinikizo kubwa la damu Shinikizo kubwa la damu linaweza kuleta madhara mbalimbali yakiwemo: • Kupasuka kwa mishipa ya damu kichwani na kusababisha kuharusi. Kiharusi ni moja ya sababu kubwa za vifo vya watu wazima  • Moyo kupanuka na hatimaye kushindwa kufanya kazi yake ya kusukuma damu.  • Kuharibika kwa mishipa ya damu kwenye figo na hatimaye figo kushindwa kufanya kazi yake ya kusafisha damu.  • Mishipa mikubwa ya damu kuharibika kwa sababu ya kuvuja kwa virutubishi vilivyo kwenye damu na kusababisha kiharusi, ugonjwa wa moyo au miguu kutopata damu ya kutosha.  Dalili ya shinikizo kubwa la damu  Wengi wa watu wenye shinikizo kubwa la damu hawana dalili zozote. Waliobaki wanaweza kuwa na dalili zifuatazo:  • Kuumwa kichwa mara kwa mara....

Yakimbie Magonjwa Sugu Yasiyoambukizwa.

Image
Tupo ndani ya mwezi wa kuadhimisha kujikinga na kupambana na magonjwa sugu yasiyoambukiza. Maadhimisho haya haswa huanza tarehe 6 hadi 13 mwezi Novemba kila mwaka ambapo hiyo wiki huwa ni kilele chake.  Lengo la maadhimisho haya ni kuifahamisha na kukumbusha jamii uwepo wa magonjwa haya hatari na kujua jinsi ya kujikinga na kuyatibu. Magonjwa yasiyoambukiza ni magonjwa yote ambayo hayawezi kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Mara nyingi huwa ni ya kudumu na ni matokeo ya muunganiko wa sababu za kijenetiki, mazingira, tabia pamoja na fiziolojia (ufanyaji kazi wa sehemu mbalimbali za mwili wa mtu).  Mfano wa magonjwa haya ni kama magonjwa ya mfumo wa mzunguko wa damu (kiharusi na mshtuko wa moyo), kisukari, saratani na magonjwa katika mfumo wa upumuaji kama vile athma (asthma). Magonjwa mengine ni kama magonjwa ya akili, majeraha, selimundu na ulemavu.  Kati ya magonjwa haya, magonjwa katika mfumo wa mzunguko wa damu yanaongoza kusababisha vifo vya watu wengi zaidi dun...

FURAHIA UNENE AU UPUNGUZE KWA STAHA

Image
Watu wengi huanza taratibu za kupunguza uzito wa mwili sababu tu wameambiwa ' aise umenenepa ' na mtu fulani au kwa sababu amevutiwa na mwenzie ambaye mwili wake ni mdogo au kuona nguo nyingi zimeshaanza kuwa ndogo au kwa sababu kasikia unene au uzito uliozidi sio salama kiafya.  Ila ukweli ni kwamba, hata kama utaweza kuyafikia malengo ya kupunguza unene/uzito wa mwili wako ni kheri kuyafikia malengo yako kwa njia sahihi ambayo itakuwezesha kudumisha uzito wa mwili wako bila kuumiza wala kukuletea madhara mwilini. NIJUE NINI KABLA YA KUANZA KUPUNGUZA UZITO WA MWILI? Ni vyema kufahamu ya kuwa kuwa na uzito uliozidi sio dhambi ingawa watu wengi hutumia muonekano wa watu wanene (ambao mara nyingi huwa na uzito uliozidi) kuwatania kwa kuwaita majina mabaya na unyanyapaa mwingine na kwa kiasi kikubwa hii ikimpata mtu ambaye hajikubali jinsi alivyo, basi hupelekea kufanya vitu vyenye madhara zaidi. 1. Tambua ya kuwa uzito wa mwili huchangiwa na sehemu kubwa mbili, sehemu...

FAHAMU KUHUSU UZITO WAKO

Image
Watu wengi hufikiria uzito uliozidi mwilini ni wingi wa mafuta tu. Kwa upande mmoja fikra hizi huchangiwa na kile wanachokiona kwa mtu husika, yaani mtu kuonekana akiwa na amejaa nyama uzembe mfano upande wa mbele wa tumbo/ kitambi (haswa wanaume ingawa siku hizi hata wanawake wanakuwa na vitambi pia) au sehemu zingine za mwili mapajani, kiunoni na kifuani.  Maana ya uzito wa mwili. Uzito wa mwili huchangiwa na mafuta, misuli, mifupa, tishu zingine zikiwa na maji au ni sawa na kusema uzito wa mtu upo katika sehemu kuu mbili, yaani uzito wenye mafuta (fat mass) na ule usiohusisha mafuta (fat free mass). Unaposema mtu ana kilogramu 50, maana yake uzito huu umechangiwa na vitu vyote vilivyotajwa hapo juu bila kuhusisha nguo wala kitu kingine chochote. Na msemo kwamba takribani 75% ya mwili wa binadamu ni maji maana yake ni kwamba asilimia hizi zinachukua sehemu yote ya uzito wa mtu, yaani asilimia zinazobaki ndio uzito halisi wa kila kinachobaki mwilini baada ya kutolewa maji ...

HAKI ZA AFYA YA UZAZI NA JINSIA

Image
HAKI ZA BINADAMU Haki za binadamu ni haki zinazohusiana na mambo ya msingi na asili ya uhuru na heshima ya ubinadamu ambapo watu wote wamepewa haki ya kupata heshima kama binadamu. Mara mtu azaliwapo mume au mke hupata haki hizi. Haki hizi zinatambuliwa kimataifa na zina usawa kwa watu wote. Nchi mbalimbali zimetia sahini na kuidhinisha haki hizi za kimataifa na kufanya ni sehemu ya sheria zao pamoja na kuweka sera zinazolinda haki hizi. HAKI ZA UZAZI Haki za uzazi ni haki zinazomwezesha mwanamke na mwanaume, mwajiriwa kutimiza majukumu yake ya uzazi na kufanya kazi bila kubaguliwa, kubugudhiwa au kupoteza ajira. Likizo ya uzazi ikiwa ni moja ya haki za uzazi, humpa mama na baba muda kutoa matunzo muhimu kwa mtoto katika siku/miezi ya mwanzo ya maisha yake, ikiwa ni pamoja na kumnyonyesha. Vilevile likizo ya uzazi humpa mama mwajiriwa muda wa kupumzika na hivyo kusaidia mwili wake kurudi katika afya na hali ya kawaida baada ya kujifungua. Haki za uzazi zina misi...

MAADHIMISHO YA SIKU YA MOYO DUNIANI

Image
Siku ya moyo duniani huadhimishwa tarehe 29 mwezi septemba kila mwaka. Shirikisho la moyo duniani ndio chimbuko la siku hii muhimu yenye lengo la kusaidia jamii kujua madhara ya magonjwa ya mfumo wa mzunguko wa damu ambapo zaidi ya nusu ya vifo vyote vitokanavyo na magonjwa yasiyo ya kuambukiza duniani husababishwa na magonjwa haya.  Hapo awali siku ya moyo duniani ilikuwa ikiadhimishwa jumapili ya mwisho ya mwezi wa tisa na kwa mara ya kwanza iliadhimishwa tarehe 24 septemba 2000. Magonjwa ya mzunguko wa damu husababisha takribani vifo vya watu milioni 17.9 dunia nzima na vifo hivi haswa huhusisha magonjwa ya moyo na kiharusi (stroke). Hii huchangia takribani asilimia 31 ya vifo vyote duniani. Moyo ni ogani ifanyayo kazi kama pampu inayosukuma damu kupitia mirija katika mwili wa binadamu na hivyo husaidia katika kusafirisha na kuzungusha virutubishi na hewa za oksijeni, kabonidayoksaidi pamoja na vitu vingine vingi. Moyo huanza kufanya kazi kuanzia siku ya 22 tangia kutung...

FAIDA ZA KUFANYA UCHUNGUZI WA KIAFYA MARA KWA MARA

Image
Faida za kufanya uchunguzi wa kiafya mara kwa mara . Kuna kampeni nyingi zinazohamasisha watu kufanya uchunguzi wa afya zao juu ya gonjwa fulani au hata juu ya hali ya afya ya mwili wote kwa ujumla. Kampeni kubwa ni za kuhamasisha kupima Virusi Vya Ukimwi (VVU) pia kupima chanzo cha homa "Sio kila homa ni Malaria". Pamoja na hayo kuna kampeni nyingi za kuhamasisha wanawake kupima hali zao afya hususani kwenye mifumo ya uzazi (saratani ya matiti na shingo ya uzazi) Licha ya jitihada nyingi za kuhamasisha watu kupima na kujua hali zao za kiafya zinazofanywa na serikali pamoja na asasi za kiraia lakini bado muamko wa watu umekuwa mdogo.  Sababu zinazofanya muamko uwe mdogo ni pamoja na hali ya uchumi, wengi kipato chao ni kidogo kiasi hata kupata milo mitatu ni mtihani.  Sababu zingine ni pamoja na uelewa mdogo juu ya umuhimu wa kuchunguza afya zao, baadhi ya Bima za Afya haziruhusu uchunguzi wa kiafya kwa asiye mgonjwa.  Utaratibu ni kwamba huwezi kupima magonjwa mbalimbali kam...

SIKU YA SICKLE CELL DUNIANI

Image
Tarehe 19 juni ni siku inayotambulika na Umoja Wa Mataifa kama siku ya selimundu duniani ambayo lengo lake ni kuhamasisha watu kitaifa na kimatataifa kutambua uwepo wa aina hii ya ugonjwa unaotokana na mapungufu ya kijenetiki. Umoja Wa Mataifa unatambua ugonjwa huu kama moja ya magonjwa ya kijenetiki unaowakumba sana watu na ni tatizo kubwa linaloathiri watu wengi katika jamii zetu. Kwa kawaida seli nyekundu za damu huwa na muonekano wa duara unaoziruhusu kufanya shughuli zake kiurahisi na kwa ufanisi mwilini. Selimundu (sickle cell disorders) huhusisha magonjwa yote ambayo huathiri seli nyekundu za damu na kuzifanya kuwa na muonekano wa mundu 🌙 (muonekano wa kikwakwa kama cha kukatia nyasi) na ugonjwa huu ni wa kurithi kwa maana kwamba mtu huupata kutoka kwa wazazi wake na hauwezi kuambukizwa kutoka kwa watu wengine tofauti na wazazi wa mtu husika.  Tafiti zinaonesha Tanzania ni moja kati ya nchi duniani ambazo kuna watoto wengi huzaliwa na magonjwa ya selimun...

MAISHA YETU YA KILA SIKU NA UCHANGIA WA DAMU.

Image
Juni 14 ni siku ya kuadhimisha kuchangia damu duniani. Siku hii hutumika kuwashukuru watu wote wanaojitolea kuchangia damu na kuhamasisha wengine ili waweze kuanza kuchangia damu. Damu hutumika kusaidia kuokoa maisha ya watu wengi sana duniani kama vile, watu waliopata ajali, wanawake wanaojifungua na watu wenye magonjwa mbalimbali kama vile upungufu wa damu mwilini (anemia). Kuchangia damu ni kitendo cha mtu kutoa damu yake ambapo huhifadhiwa katika mfuko maalum (blood bag) na kuwekwa katika joto kati ya nyuzi joto (°c) +2 hadi +6. Joto hilo ni sahihi katika kuhakikisha vitu vilivyomo ndani ya damu kama vile seli nyekundu, chembe sahani na vinginevyo haviharibiwi na damu haishambuliwi na vijidudu hatari kama vile bakteria na virusi. Tujikumbushe vitu vichache kuhusu damu na kuchangia damu Damu ni moja kati ya tishu katika miili ya wanyama (binadamu) ambayo hutumika kusafirisha virutubishi, takamwili, oksijeni, homoni na vitu vingine mwilini..Uwepo wa seli nyekundu za damu ...

TUNAWEZA ISHI BILA TUMBAKU.

Image
Tarehe 31 Mei ya kila mwaka ni siku ya kupinga matumizi ya sigara na bidhaa za Tumbaku Duniani (World No Tobacco Day). Siku hii iliasisiwa na Shirika La Afya Duniani (WHO) mwaka 1987. Hii ni kutokana na madhara ya bidhaa hizo kwa watumiaji na watu wanaowazunguka kiafya na kimazingira. Madhumuni ya siku hii ni kuhamasisha watu na kutoa elimu juu ya madhara yatokanayo na uvutaji na utafunaji wa tumbaku. Utengenezaji na uvutaji wa sigara ni  halali hapa nchini kwetu Tanzania. Utafiti unaonyesha kwa siku duniani watu takribani 500 hufariki dunia kutokana na matumizi ya tumbaku. Tumbaku inaweza kuzalisha aina mbalimbali za saratani, magonjwa ya moyo, kiharusi, vidonda vya tumbo na magonjwa sugu ya kifua. Utafiti uliofanywa hapa nchini unaonyesha asilimia 40 hadi 50 ya watu wanaougua ugonjwa wa saratani ya mapafu unatokana na uvutaji wa tumbaku. Katika hilo hata wasiotumia tumbaku wamekuwa wakiathirika zaidi kutokana na kuvutishwa bila ridhaa yao, kutokana na ukwe...

Siku Ya Hedhi Salama

Image
Tarehe 28 mwezi mei kila mwaka ni siku ya kuazimisha siku ya hedhi salama duniani (safe menstrual day) Kwa kifupi tujikumbushe mambo machache kuhusu hedhi  Hedhi ni kipindi ambacho wanawake waliokwisha balehe hupitia ambapo huambatana na kutokwa na damu, na kwa kawaida huwa mara moja kwa mwezi..Na hii hutokea kwa sababu mji wa mimba (yuterasi-uterus) unakuwa umeandaliwa tayari kwa kupokea na kulea mimba, maandalizi haya huusisha kuongezeka kwa unene wa misuli ya yuterasi na mishipa ya damu. Pale ambapo mwanamke asiposhika mimba, ukuta wa mji wa mimba huachia au kudondoka (shading of uterus wall) na hii ndio hupelekea kutokwa na damu katika kipindi hiki ambacho kwa kawaida huchukua takribani siku 3 hadi 8, ingawa inaweza kutokea mwanamke kupata hedhi kwa muda zaidi ya siku nane kutokana na sababu mbalimbali. Kwa wanawake wengi hedhi hutokea kwa namna ambayo wao huijua na wanaweza kujua ni siku gani katika mwezi huziona siku zao ( kwenda mwezini kama inavofaha...