COVID19 na Vitamini D
Habari za saa hizi mpendwa msomaji wa makala zetu! Ni matumaini yetu unaendelea vizuri kiafya na upo wima katika mapambano dhidi ya Corona kwa kuchukuwa tahadhari zote muhimu kujilinda na kuwalinda waliokunzunguka msipate maambukizi. Leo tutaongelea juu ya Vitamini D dhidi ya Corona. Hadi sasa kuna tafiti nyingi kuhusu ugonjwa huu wa Covid 19 zimefanyika na zinaendelea kufanyika na tafiti hizi hutofautiana hasa katika kuhusianisha ugonjwa huu na vitu kadha wa kadha. Ingawa CHAKULA (Lishe na Virutubishi) ni moja kati ya vitu ambavyo vimekuwa vikizungumziwa na kufanyiwa utafiti kwa kiasi kikubwa sehemu mbalimbali ulimwenguni tangu mlipuko wa ugonjwa huu uanze disemba 2019 huko China.. Hapa kwetu Tanzania kumekuwa na msisitizo mkubwa kutoka kwa wataalamu wa afya na lishe kuhusu ulaji wa Vyakula vyenye Vitamini C kwa wingi kama vile malimao, machungwa, tangawizi, mananasi, vitunguu swaumu, ndimu, mboga za majani kama vile giligilani, bila kusahau mapera (yaliyosahaulika na wat