DHANA ZA MAHUSIANO KATI YA MZAZI NA MTOTO KATIKA MALEZI.
Tangu zamani kumekuwa na dhana na fikra mbalimbali katika jamii juu ya ukaribu wa mzazi na mtoto katika malezi na makuzi. Fikra na dhana hizi bado zipo kwenye jamii zetu kati ya familia na familia. Wapo wanaoamini mzazi hapaswi kuwa na urafiki na mtoto. Mzazi akiwa na urafiki na mtoto kuna mfanya mtoto awe kiburi na dharau kwa watu wengine kwa kuwa anajua mzazi ni rafiki yake atamtetea. Na muda mwingine urafiki huo hujenga mazoea kisha mtoto huwa na dharau kwa mzazi husika "Mazoea huleta dharau". Dhana hii ni kubwa na maarufu sana kwenye familia nyingi za Kiafrika. Baba awe Baba na sio rafiki wa mtoto, baba inabidi aogopwe na kuheshimiwa sana na mtoto na sio mtoto akimuona baba aanze kumchezeachezea. Ni hii dhana ambayo wazazi wetu wengi wamekulia na imejenga nidhamu kubwa kati yao kwa kuwa kuna mstari mwekundu ulikolezwa (Red bold line) kati ya mtoto na mzazi. Pia kundi lingine linabeba dhana ya MZAZI LAZIMA UWE RAFIKI MKUBWA WA MWANAO. Kundi hili l