FAIDA ZA MAZIWA YA MAMA KWA MTOTO
FAIDA ZA MAZIWA YA MAMA KWA MTOTO Maziwa ya matiti ni maziwa yanayotolewa na mama ili kumnyonyesha mwanawe. Maziwa hayo hutoa chanzo msingi cha lishe kwa watoto kabla ya wao kupata uwezo wa kula vyakula vingine, yaani watoto wachanga hadi umri kadri wanavyoweza kuendelea kunyonyeshwa. Kunyonyesha ni tendo la kumpa mtoto maziwa kutoka katika titi la mama moja kwa moja au kumnywesha mtoto maziwa ya mama yakikamuliwa kwa kutumia kikombe. Maziwa ya mama ndiyo chakula bora kwa mtoto mchanga kuliko maziwa wengine au chakula kingine. Shirika la Afya duniani (WHO) linapendekeza mtoto kunyonyesha maziwa ya mama pekee kwa miezi sita ya kwanza ya maisha, vyakula vizito huanzishwa mnamo umri huu unapoongezeka, hatua kwa hatua wakati ishara ya utayari huonekana, kunyonyesha huendelea kupendekezwa kama nyongeza mpaka angalau miaka miwili, au kwa muda mrefu jinsi mama na mtoto watakavyotaka. Maziwa ya mama ni chakula na kinywaji cha kwanza, na cha pekee kwa mtoto tangu anapozaliwa mpa...