Posts

Showing posts from July 24, 2020

UZITO ULIOKITHIRI

Image
UNENE AU UZITO ULIOKITHIRI NI HATARI  Kuwa na unene au uzito uliokithiri ni chanzo cha matatizo mengi ya kiafya hasa magonjwa yasiyo yakuambukizwa kama vile; kisukari, saratani na shinikizo kubwa la damu.  Takwimu zinaonyesha zaidi ya watu bilioni mbili duniani wameathiriwa na fetma (obesity) na zaidi ya vifo milioni nne vinasababishwa na fetma.   Katika nchi ya Tanzania takwimu za vifo vinavyotokana na magonjwa yasiyo yakuambukizwa (NCD) kutoka katika Shirika la Afya duniani (WHO) zinaonyesha vifo 134,600 kwa mwaka hutokana na magonjwa yasiyo yakuambukizwa (NCD), ambayo ni sawa na asilimia thelathini na tatu (33%) ya vifo vyote, hutokana na magonjwa yasiyoyakuambukizwa, na vifo hivi vimekuwa vikiongezeka kila mwaka   Kitaalamu njia ambayo ni salama zaidi mtu anapotaka kupunguza uzito au unene ni ile inayohusisha ulaji sahihi wa vyakula unaozingatia kanuni, ufanyaji wa mazoezi na kanuni mbalimbali za afya ambazo zimekuwa zikielezewa mara kwa mara na wataalamu wa