SIKU YA WATU WENYE UALBINO DUNIANI.
Siku ya watu wenye ualbino duniani Ualbino ni hali ambayo husababishwa na kurithi jeni (genes) kutoka kwa wazazi wote wawili ambapo mtoto hukosa melanini (rangi ya asili-pigmentation). Rangi ya asili hukosekana katika macho, ngozi, nywele na kupelekea kuwa na uoni hafifu na kuwa katika hatari ya kupata saratani ya ngozi. Ikumbukwe kwamba wazazi wote wanaweza wasiwe na ualbino lakini kama walibeba jeni za ualbino, hii ndio hupelekea wao kupata mtoto mwenye ualbino kwa maana kwamba wao walibeba tu zile jeni ila hazikuoneshwa katika maumbile. Barani Afrika Tafiti zinaonesha kuwa idadi ya watu wanaoathirika na ualbino ni kubwa kusini mwa jangwa la sahara ambapo kwa Tanzania inakadiliwa mtu 1 kati ya 1400 ana ualbino, kwa utafiti uliofanyika nchini zimbabwe ulionesha mtu mmoja kati ya 1000 ana ualbino. Ni vyema kukumbuka pia ualbino hutokea kwa viumbe wengine kama vile mbwa, simba, tembo, taiga na wanyama wengine wengi. Baadhi ya changamoto ambazo watu we