SIKU YA KUPINGA WATU KUJIUA DUNIANI.
Wanaojiua wote ni wajinga? Kujiua ni kuandamwa na roho mbaya ya mauti? Kujiua ni kujiadhibu tu? Kujiua ni kufanya maamuzi kwa kukurupu.... Kujiua ni kufika mwisho wa kufikiri... Kila mmoja anaongea lake juu ya anachokiona ni sawa pale anaposikia mtu kajiua. Bila kujali fikra zote hizo, ukweli ni kwamba watu wanajiua sana. Kwa takrimu kwa kila sekunde 40 mtu mmoja hujiua duniani. Ukipiga mahesabu hapo kwa harakaharaka kwa wiki watu 630 hujiua duniani. Chanzo ni nini? Wapo wanaojiua na kuacha ujumbe wa sababu za kwanini wametoa uhai wao, na wapo ambao hujiondoa tu bila kuacha ujumbe wowote juu ya nini kimepelekea maamuzi yake hayo. Wote kwa pamoja huacha simanzi kubwa kwa wapendwa wao. Sababu ya ugumu wa maisha, sababu ya matatizo ya akili, sababu ya magonjwa sugu, sababu ya msongo wa mawazo usiohimilika kama vile aibu baada ya kufanyiwa tendo baya, sababu ya mapenzi, sababu ya ugaidi na kisasi ni sababu maarufu kati ya sababu nyingi zinazopelekea watu kujiny...