SIKU YA KUPINGA WATU KUJIUA DUNIANI.
Wanaojiua wote ni wajinga?
Kujiua ni kuandamwa na roho mbaya ya mauti?
Kujiua ni kujiadhibu tu?
Kujiua ni kufanya maamuzi kwa kukurupu....
Kujiua ni kufika mwisho wa kufikiri...
Kila mmoja anaongea lake juu ya anachokiona ni sawa pale anaposikia mtu kajiua. Bila kujali fikra zote hizo, ukweli ni kwamba watu wanajiua sana.
Kwa takrimu kwa kila sekunde 40 mtu mmoja hujiua duniani. Ukipiga mahesabu hapo kwa harakaharaka kwa wiki watu 630 hujiua duniani.
Chanzo ni nini?
Wapo wanaojiua na kuacha ujumbe wa sababu za kwanini wametoa uhai wao, na wapo ambao hujiondoa tu bila kuacha ujumbe wowote juu ya nini kimepelekea maamuzi yake hayo. Wote kwa pamoja huacha simanzi kubwa kwa wapendwa wao.
Sababu ya ugumu wa maisha, sababu ya matatizo ya akili, sababu ya magonjwa sugu, sababu ya msongo wa mawazo usiohimilika kama vile aibu baada ya kufanyiwa tendo baya, sababu ya mapenzi, sababu ya ugaidi na kisasi ni sababu maarufu kati ya sababu nyingi zinazopelekea watu kujinyonga.
Ukiziangalia na kuzitafakari hizo sababu utaona kama hazina uzito kiasi cha mtu kujitoa uhai. Lakini cha kwanza jua tunatofautiana namna za kuhimili changamoto za maisha. Kwa tofauti hizo wengine huweza kuhimili kwa muda mfupi, wengine muda mrefu na wengine muda kiasi. Tunatofautiana mitazamo ya kusuluhisha matatizo, wapo wanaopenda wanaoweza kujadili na wengine na kufikia muafaka, wapo naoapenda kuhifadhi tu ndani ya mioyo yao mpaka njia itakapotokea. Na wapo ambao ni wepesi kupuuzia matatizo yao (hana habari)
Tukiachana na tofauti zetu mbalimbali turudi kwenye dhumuni kunwa la siku ya leo. Lengo la siku ya leo ni kupunguza au kuzuia watu kujiua
Kwanza kabisa jamii yetu nzima yatupasa kuwa pamoja na kuwa katika masikilizano. Jamii iwasogeze karibu wale wote wanaojitenga au wenye ukimya wajihisi ni sehemu ya jamii na wawe wepesi kuelezea lolote gumu wanalopitia
Jamii ifundishwe kubaini mabadiliko ya mtu kitabia yatayoweza msababisha kujiua. Mabadiliko kama mtu kuwa mlevi mno au uraibu mkubwa sana baada ya kupatwa tatizo. Tabia za kujitenga na wengine wakati akiwa na matatizo.
Lakini juu ya yote mazingira rafiki ya maisha mazuri ni muhimu kuwekwa. Mifumo ya afya ya akili, huduma za kijamii na kiroho, suala la elimu isiyokandamizi, uwepo wa ajira na elimu ya mahusiano. Ni ukosefu wa hivyo vitu uliosababisha watu wengi kujiua sehemu mbalimbali za dunia.
Na
Nobel Edson
Fasmo Tanzania
Comments