Shairi: TUISHINDE CHUKI
Tuishinde Chuki
Nasaha lukuki,
Leo tusemezane,
Tuishinde chuki,
Mbinu tupeane,
Isilete taharuki,
Mwisho tuuane.
Chuki roho chafu,
Hasara abadani,
Watu waliodhaifu,
Huitunza kifuani,
Tabia ya siafu,
Kujitia hatiani.
Chuki mitaani,
Imefika bungeni,
Imeingia kanisani,
Upendo pembeni,
Tupendane jamani,
Itasaidia mbeleni.
Alimchukia Sadiki,
Akapanga mpoteza,
Kumvamia alidiriki,
Ghafla akateleza,
Akapoteza umiliki,
Sasa magereza.
Chuki huleta aibu,
Hilo jambo jua,
Waumbuka kiajabu,
Waangukia pua,
Utaishi kwa taabu,
Utawaza jiua.
Ndugu twachukiana,
Sisi kwa sisi,
Kutwa twawindana,
Twaishi kifisi,
Twashindwa samehana,
Tumejawa ubinafsi.
Samehe mara sabini,
Na ukiweza sahau,
Zinashauri dini,
Kumbuka hilo mdau,
Tukirudi vumbini,
Upendo utawale walau.
Tusamehane ndugu,
Chuki ndani ondoa,
Yaweza geuka rungu,
Kisha uhai ikakutoa,
Haimpendezi Mungu,
Hakika yatutia doa.
Na
Nobel Edson Sichaleh
Fasmo Tanzania
Comments