MAZINGIRA NA DUNIA YETU
Mazingira ni wewe na mimi, mawe, miti, anga wanyama na kila kitu tunachokiona na tusichokiona kama vile vijidudu ambavyo vinaweza kuonekana kwa msaada wa vifaa maalumu vya maabara. Mazingira ndio chanzo cha hali ya hewa, chakula, hewa tunayoivuta (oksijeni), maji tunayokunywa na vitu vingine kede kede vyenye manufaa kwetu.. Vitu vyote katika mazingira hutegemeana. Kwa namna kwamba viumbe hai hutegemea viumbe hai wengine na visivyo hai ili maisha yaende. Kwa namna hii kunakuwa na matumizi ya vitu katika mazingira kwa namna fulani ambayo inaweza ikawa inafaa au ikawa isiyofaa. Kwa mfano binadamu hutumia mimea (miti) kama kuni au kutengeneza mkaa kwa ajili ya nishati ya kutumia majumbani na sehemu zingine, lakini tumeshafika mahali ambapo matumizi ya miti kwa ajili ya shughuli kama hizi na nyingine nyingi yamepelekea kuharibika na kupotea kwa uoto asili na kupelekea madhara katika hali ya hewa, mfano kuongezeka kwa jotoridi na kupungua kwa kiasi cha mvua duniani.. ...