UJINGA UNAUA
Kwakuwa wote tunazaliwa na kufa. Na kwa imani zetu wengi tunaamini sisi ni wa Mungu. Kwenye maandiko Mungu anasema, Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa" Kwa haraka maana yake duniani kuna maadui wa wanadamu ambao ili mwanadamu asiangamizwe ni vyema awe na maarifa, yaani asiwe mjinga. Ujinga unaangamiza na kuua kama maarifa hayatatumika kunusuru hiyo hali. Kuna hadithi nyingi za kweli za watu waliofia kwenye nyumba za waganga wakienyeji kwa ugonjwa unaotibika hospitali. Kuna hadithi nyingi za watu waliokufa wakiwa wanautafuta utajiri kwa njia zisizohalali, bila shaka hata wewe unayo hadithi ya mtu au watu waliopoteza maisha kwa ajari ambayo ingeweza kuepukika kama taratibu zote stahiki zingefuatwa. Waliotangulia tunawaombea Mungu awalaze kwa amani ila hadithi za chanzo na mazingira ya vifo vyao kwetu ni somo katika kuzuia vifo namna ile visijirudie. Kwakuwa kuna maadui wengi na wenye njia mbalimbali za kutushambulia na kuhakikisha tunadhohofika kiuch...