UJINGA UNAUA

Kwakuwa wote tunazaliwa na kufa. Na kwa imani zetu wengi tunaamini sisi ni wa Mungu. Kwenye maandiko Mungu anasema, Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa"
Kwa haraka maana yake duniani kuna maadui wa wanadamu ambao ili mwanadamu asiangamizwe ni vyema awe na maarifa, yaani asiwe mjinga.

Ujinga unaangamiza na kuua kama maarifa hayatatumika kunusuru hiyo hali. Kuna hadithi nyingi za kweli za watu waliofia kwenye nyumba za waganga wakienyeji kwa ugonjwa unaotibika hospitali. Kuna hadithi nyingi za watu waliokufa wakiwa wanautafuta utajiri kwa njia zisizohalali, bila shaka hata wewe unayo hadithi ya mtu au watu waliopoteza maisha kwa ajari ambayo ingeweza kuepukika kama taratibu zote stahiki zingefuatwa. Waliotangulia tunawaombea Mungu awalaze kwa amani ila hadithi za chanzo na mazingira ya vifo vyao kwetu ni somo katika kuzuia vifo namna ile visijirudie.

Kwakuwa kuna maadui wengi na wenye njia mbalimbali za kutushambulia na kuhakikisha tunadhohofika kiuchumi,kijamii,kiafya na kimaisha kwa ujumla ni vyema kutoacha kujifunza mbinu mpya na maarifa mapya ya kupambana na maadui hao. Moja ya waasisi wa taifa letu Baba wa Taifa, Mwl Julius Nyerere alitaja UMASKINI, UJINGA na MARADHI ndio maadui wa taifa hili. Akimaanisha uwepo wa hawa maadui ndio chanzo cha sisi kutopiga hatua kubwa za kimaendeleo kwani kuna upungufu wa nguvu inayosababishwa na uwepo wa vifo vinavyotokana na maradhi. Kama taifa tuna uhaba wa wataalam na ujuzi wa kuendesha sekta mbalimbali na kutuletea maendeleo kutokana na watu wengi kutokuwa na elimu. Pia Umaskini unasababisha tunashindwa kupambana na maadui wengine pia tunashindwa kuinuka kitechnolojia ili kuongeza uzalishaji ambao utaleta tija kwenye maendeleo yetu.

Kuna siku nikafungulia redio kusikiliza taarifa ya habari nikasikia.... WIVU WA MAPENZI WASABABISHA MWANAUME MMOJA KUMUUA MPENZI WAKE KWA BUNDUKI KISHA NA YEYE KUJINYONGA. Ni kitu gani kilichomuua huyo dada. Kati ya Bunduki, Wivu wa Mapenzi na huyo mwanaume ni nani aliyemuua huyo dada? 
Hiyo taarifa ilinipelekea kuona upande mwingine wa mambo ambavyo huwa. Na ndiyo hivyo ambavyo Ujinga husababisha vifo na kusimama kama Wivu wa Mapenzi kwenye hiyo taarifa.
ÀMKA TAFUTA MAARIFA
UJINGA UNAUA!

By Nobel Edson Sichaleh
Mwenyekiti
0783961492

Comments

Popular posts from this blog

Mitindo Yetu Ya Ulaji.

Nafasi ya Maziwa katika Afya Zetu.

MADHARA YA UTENGANO WA KIJAMII YALIYOSABABISHWA NA COVID19