Shairi: IWAJE?

Wewe ulitakaje?
Shule za msingi
Vitu vifanyikaje?
Katikati ya vipindi
Watoto walaje?
Kwa elimu-ushindi

Mimi kama wewe
Nina uwezo kufikiri
Nafikiri mwenyewe
Siwezi shikiwa akili
Mwenye haki apewe
Vinginevyo ni ukatili

Haki ya kuelimika
Na malezi stahiki
Hakizo kuzishika
Mtoto huwa rafiki
Mzaziye wajibika
Utajaona mantiki

Mapumziko wasile!
Darasani waingie
Njaa iwazingile
Somo lisiwaingie
Shule waikimbie
Maoniyo niambie?

Wale chakula vizuri
Darasa changamfu
Wasipate tena sifuri
Utoro ugeuke hafifu
Wawe watoto wazuri
Wenye afya nadhifu.

Changia mawazo
Tupate mwongozo
Tuwajengee uwezo
Elimu bora ni nguzo
Hatua hizi mwanzo
Tuvishinde vikwazo

Comments

Popular posts from this blog

Mitindo Yetu Ya Ulaji.

Nafasi ya Maziwa katika Afya Zetu.

MADHARA YA UTENGANO WA KIJAMII YALIYOSABABISHWA NA COVID19