UMUHIMU WA KUSOMA MABANDIKO YA LISHE KWA MLAJI
UMUHIMU WA KUSOMA MABANDIKO YA LISHE KWA MLAJI Mabandiko ya lishe ni maandishi yanayompatia mlaji taarifa mbalimbali juu ya bidhaa na thamani ya lishe inayo patikana kwenye chakula ambacho anataka kununua, mabandiko ya lishe huwa yanaandikwa haswa kwenye vyakula ambavyo vipo katika vifungashio mbalimbali kama vile chupa za maji, mifuko ya maziwa na juisi. Taarifa zinazowekwa kwenye mabandiko ni pamoja na kiasi cha kutumika ,idadi ya kalori, kiasi cha mafuta, virutubishi vinavyo patikana pamoja, ujazo wa chakula, muda wa matumizi, kanuni za matumizi na viungo viivyotumika katika kutengeneza chakula husika. Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ni shirika ya kiserikali ambalo linasimamia ubora, usalama wa chakula kwa mlaji. Kila bidhaa ya chakula kabla haijaingia sokoni na kumfikia mlaji ni lazima kwanza ihakikiwe ubora wake kwa matumizi, jinsi ilivyo tengenezwa, usalama wake na kisha kubandikwa mabandiko ya lishe ili kumsaidia mla...