UMUHIMU WA KUSOMA MABANDIKO YA LISHE KWA MLAJI

UMUHIMU WA KUSOMA MABANDIKO YA LISHE KWA MLAJI
                                               
Mabandiko ya lishe ni maandishi yanayompatia mlaji taarifa mbalimbali juu ya bidhaa na thamani ya lishe inayo patikana kwenye chakula ambacho anataka kununua, mabandiko ya lishe huwa yanaandikwa haswa kwenye vyakula ambavyo vipo katika vifungashio mbalimbali kama vile chupa za maji, mifuko ya maziwa na juisi. Taarifa zinazowekwa kwenye mabandiko ni pamoja na kiasi cha kutumika  ,idadi ya kalori, kiasi cha mafuta, virutubishi vinavyo patikana pamoja, ujazo wa chakula, muda wa matumizi, kanuni za matumizi na viungo viivyotumika katika kutengeneza chakula husika.

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ni shirika ya kiserikali ambalo linasimamia ubora, usalama wa chakula kwa mlaji. Kila bidhaa ya chakula kabla haijaingia sokoni na kumfikia mlaji ni lazima kwanza ihakikiwe ubora wake kwa matumizi, jinsi ilivyo tengenezwa, usalama wake na kisha kubandikwa mabandiko ya lishe ili kumsaidia mlaji kujua bidhaa anayoinunua.

Ni taarifa gani unaweza kuzipata kwenye mabandiko ya lishe 
●Jina la bidhaa unayotaka kununua.
●Chapa ya bidhaa.
●Aina ya viungo vilivyotumika na kwa kiasi gani.
●Taarifa za lishe kama vile kiwango cha mafuta, madini, aina za vitamini, protini, kalori zinazopatikana kwenye chakula husika.
●Maandiko ya tarehe bidhaa ilipo tengenezwa na na maandiko ya tarehe ya kumalizika muda wake.

Jinsi ya kusoma mabandiko ya lishe kwenye chakula
1.Anza kwa kuangalia ukubwa wa kutumika,
Angalia kiasi ambacho anatakiwa kula mtu mmoja ,mfano kikombe kimoja kwa mtu mmoja. Hivyo kula zaidi ya kikombe kimoja itakupelekea kupata kalori na virutubishi vingine kama vile mafuta na sukari zaidi ya vile inavyotakiwa kupata.hivyo kupelekea kuongezeka kwa uzito au kupata matatizo mengine ya kiafya.
                                              
2. Angalia jumla ya kalori  utakazo zipata kwa kula chakula husika.

3. Chagua vyakula venye kiwango kidogo cha mafuta ,sukari na chumvi
Hii inasaidia kupunguza kupata magonjwa yasioambukiza kama vile unene uliopitiliza, shinikizo la damu, na magonjwa ya moyo.
4. Chagua vyakula vitakavyo kupatia vitamin, madini na nyuzinyuzi kwa wingi.

5. Angalia kama kuna virutubisho vyovyote vilivyoongezwa kwenye chakula husika.
Mfano vitamin A kwenye mafuta ya kula na iodine kwenye chumvi.

Umuhimu wa mabandiko Ya lishe kwa mlaji
Mabandiko ya lishe yana umuhimu mkubwa sana kwa mlaji, na ndio maana hata serikali ikaamua kuanzisha taasisi za kuhakikisha mlaji anapata taarifa mbalimbali za bidhaa kwa ustawi wa afya yake na jamii kwa ujumla.
Zifuatazo ni faida au umuhimu wa mabandiko ya lishe kwa mlaji.

■Mabandiiko ya lishe yanasaidia kuhamasisha ulaji sahihi kwa mlaji.
Kutokana na kuwa mabandiko ya lishe yanamuonyesha mlaji kiwango cha kalori na virutubishi vilivyopo kwenye chakula , hivyo kumsaidia mlaji kujua ni chakula kipi kizuri au kibaya kwa afya yake hivyo kumfanya mlaji kuwa na maamuzi sahihi ya namna gani ale.

■Mabandiko ya lishe humsaidia mlaji mwenye mahitaji binafsi ya kiimani 
 Taarifa za kwenye mabandiko ya lishe pia yanaonyesha viungo vilivyotumika kutengeza chakula, hivyo kumsaidia mlaji kujua ni kitu gani ambacho hatumii kuligana na imani yake au mahitaji yake ya mwili. Kwa mfano mtu kutochagua chakula chenye kemikali, au chakula ambacho kimepikwa kwa mafuta ya kitimoto nk

■Mabandiko ya lishe yanamsaidia mlaji mwenye mahitaji maalumu ya kiafya(matibabu) kujua ni chakula kipi anapaswa kununua.
Kama vile watu wenye alegi na baadhi ya viungo kama vile karanga, maziwa, mayai nk.pia kwa watu wenye magonjwa kama vile kisukari wanahitaji vyakula maalumu kwa mfano biskuti na soda zisizo na sukari ,hivyo kwa mlaji kusoma mabandiko ya lishe yanamsaidia kujua ni bidhaa gani anunue.

■Mabandiko ya lishe pia yanamsaidia mlaji kufanya maamuzi sahihi juu ya bidhaa ipi anunue kwa faida ya afya yake.
Kwa kusoma viungo vilivyotumika inamsaidia mlaji kujua kati ya bidhaa nyingi zilizopo ipi anunue.
Kwa mfano maandazi yaliyookwa yana mafuta kidogo ukilinganisha na maandazi ya kukaanga.

USILE CHAKULA PUNGUFU BALI KULA CHAKULA SAHIHI KWA KUSOMA MABANDIKO YA LISHE .

Imeandaliwa na
Norah Mwacha.
Mtaaluma wa Lishe.
Fasmo Tanzania.
0710487663.

Comments

Popular posts from this blog

Mitindo Yetu Ya Ulaji.

Nafasi ya Maziwa katika Afya Zetu.

MADHARA YA UTENGANO WA KIJAMII YALIYOSABABISHWA NA COVID19