HAKI ZA MGONJWA POPOTE PALE
HAKI ZA MGONJWA Katika maisha kwa sababu mbalimbali mwanadamu hupatwa na udhaifu wa mwili hivyo hujikuta akitafuta tiba kwenye taasisi za kutolea tiba za afya. Taasisi hizo hutoa huduma mbalimbali na katika kupokea huduma mgonjwa huwa na haki zifuatazo ● Haki ya kusikilizwa ●Mgonjwa ana haki ya kujua huduma za afya zinazotolewa katika hospitali, ikiwa ni pamoja na mkalimani endapo mgonjwa haimudu lugha ya kawaida katika eneo hilo. ●Haki ya kutaka gonjwa lake liwe siri ●Haki ya kuulizia na kuambiwa majibu ya vipimo vyake ●Haki ya kukataa kuendelea na matibabu ●Haki ya kuomba abadilishiwe mtalaamu (Daktari/Muuguzi) ● Mgonjwa ana haki ya kujua ni nani anayetoa huduma za matibabu na ni nani anayehusika na kumuhudumia.. ●Haki ya kupewa elimu ya kujikinga au kujiepusha na magonjwa ●Haki ya kupewa ufafanuzi toshelezi juu ya matumizi ya dawa ●Haki ya kupewa ufafanuzi wa gharama za matibabu yake ●Haki ya kuhudumiwa kama wagonjwa wengine bila ...