HAKI ZA MGONJWA POPOTE PALE

HAKI ZA MGONJWA

Katika maisha kwa sababu  mbalimbali mwanadamu hupatwa na udhaifu wa mwili hivyo hujikuta akitafuta tiba kwenye taasisi za kutolea tiba za afya. Taasisi hizo hutoa huduma mbalimbali na katika kupokea huduma mgonjwa huwa na haki zifuatazo

Haki ya kusikilizwa
●Mgonjwa ana haki ya kujua huduma za afya zinazotolewa katika hospitali, ikiwa ni pamoja na mkalimani endapo mgonjwa haimudu lugha ya kawaida katika eneo hilo.
●Haki ya kutaka gonjwa lake liwe siri
●Haki ya kuulizia na kuambiwa majibu ya vipimo vyake
●Haki ya kukataa kuendelea na matibabu
●Haki ya kuomba abadilishiwe mtalaamu (Daktari/Muuguzi)
Mgonjwa ana haki ya kujua ni nani anayetoa huduma za matibabu na ni nani anayehusika na kumuhudumia..
●Haki ya kupewa elimu ya kujikinga au kujiepusha na magonjwa
●Haki ya kupewa ufafanuzi toshelezi juu ya matumizi ya dawa
●Haki ya kupewa ufafanuzi wa gharama za matibabu yake
●Haki ya kuhudumiwa kama wagonjwa wengine bila kujali kabila, rangi ya ngozi, ulemavu wowote au muonekano.
●Haki ya Matibabu sahihi ya Tiba na huduma za kibinadamu.
●Haki ya kukataa ushiriki katika utafiti wa kitabibu.
●Haki ya imani ya dini.
Mgonjwa ana haki ya kukataa matibabu yeyote ambayo yatakuwa yanavunja misingi ya imani yake ya dini
●Haki ya Kufundishwa Haki na Jukumu Lake kama Mgonjwa.
Haki ya kutoa malalamiko yake juu ya huduma za afya
●Haki ya Mawasiliano na Kupokea Wageni.
Mgonjwa ana haki ya kuwasiliana na ndugu na jamaa wengine na kupokea wageni chini ya mipaka inayofaa iliyowekwa na sheria na kanuni za taasisi ya huduma ya afya .
●Haki juu Rekodi za Matibabu. - Mgonjwa anastahiki muhtasari wa historia yake ya matibabu na hali  yake ana haki ya kuona yaliyomo kwenye rekodi zake za matibabu.
Watoa huduma za afya wanajua HAKI ZA WAGONJWA ila wagonjwa huwa kwa wingi na kwa ukubwa hawajui HAKI ZAO hivyo kuhudumiwa na kuona wanastahili yote wanayoyapitia wakati wa kutafuta tiba wakati kuna vingine ni nje ya haki zao.

Na
Nobel Edson Sichaleh
Consumer Scientist
Fasmo Tanzania
0783961492

Comments

Popular posts from this blog

Mitindo Yetu Ya Ulaji.

Nafasi ya Maziwa katika Afya Zetu.

MADHARA YA UTENGANO WA KIJAMII YALIYOSABABISHWA NA COVID19