FURAHIA UNENE AU UPUNGUZE KWA STAHA
Watu wengi huanza taratibu za kupunguza uzito wa mwili sababu tu wameambiwa ' aise umenenepa ' na mtu fulani au kwa sababu amevutiwa na mwenzie ambaye mwili wake ni mdogo au kuona nguo nyingi zimeshaanza kuwa ndogo au kwa sababu kasikia unene au uzito uliozidi sio salama kiafya. Ila ukweli ni kwamba, hata kama utaweza kuyafikia malengo ya kupunguza unene/uzito wa mwili wako ni kheri kuyafikia malengo yako kwa njia sahihi ambayo itakuwezesha kudumisha uzito wa mwili wako bila kuumiza wala kukuletea madhara mwilini. NIJUE NINI KABLA YA KUANZA KUPUNGUZA UZITO WA MWILI? Ni vyema kufahamu ya kuwa kuwa na uzito uliozidi sio dhambi ingawa watu wengi hutumia muonekano wa watu wanene (ambao mara nyingi huwa na uzito uliozidi) kuwatania kwa kuwaita majina mabaya na unyanyapaa mwingine na kwa kiasi kikubwa hii ikimpata mtu ambaye hajikubali jinsi alivyo, basi hupelekea kufanya vitu vyenye madhara zaidi. 1. Tambua ya kuwa uzito wa mwili huchangiwa na sehemu kubwa mbili, sehemu