FAHAMU KUHUSU UZITO WAKO
Watu wengi hufikiria uzito uliozidi mwilini ni wingi wa mafuta tu. Kwa upande mmoja fikra hizi huchangiwa na kile wanachokiona kwa mtu husika, yaani mtu kuonekana akiwa na amejaa nyama uzembe mfano upande wa mbele wa tumbo/ kitambi (haswa wanaume ingawa siku hizi hata wanawake wanakuwa na vitambi pia) au sehemu zingine za mwili mapajani, kiunoni na kifuani. Maana ya uzito wa mwili. Uzito wa mwili huchangiwa na mafuta, misuli, mifupa, tishu zingine zikiwa na maji au ni sawa na kusema uzito wa mtu upo katika sehemu kuu mbili, yaani uzito wenye mafuta (fat mass) na ule usiohusisha mafuta (fat free mass). Unaposema mtu ana kilogramu 50, maana yake uzito huu umechangiwa na vitu vyote vilivyotajwa hapo juu bila kuhusisha nguo wala kitu kingine chochote. Na msemo kwamba takribani 75% ya mwili wa binadamu ni maji maana yake ni kwamba asilimia hizi zinachukua sehemu yote ya uzito wa mtu, yaani asilimia zinazobaki ndio uzito halisi wa kila kinachobaki mwilini baada ya kutolewa maji ...