NILISHE NIFAULU
NILISHE NIFAULU Ni mradi unaotekelezwa na asasi isiyokuwa ya kiserikali ya FASMO ikishirikiana na wanajamii. Mradi huu umelenga utoaji wa chakula katika shule za msingi kama njia kuu ya kuchochea mahudhurio na utulivu wakati wa kujifunza ambavyo kwa pamoja huchangia matokeo bora (ufaulu) kwa wanafunzi na shule kwa ujumla. Familia nyingi za Kitanzania zina uwezo mdogo wa kiuchumi. Watoto hulazimika kuamka asubuhi sana na kukimbilia shule bila kupata kitu chochote cha kula. Na kwa bahati mbaya hata shuleni hakuna utaratibu wa ugawaji wa chakula hivyo mtoto hujikuta masaa zaidi ya saba hajapata chakula kwa kuwa hata hela ya matumizi shuleni hajapewa au ni ndogo sana. Uelewa wa wanafunzi huwa hafifu kutokana na mazingira hayo ya ukosefu wa chakula wakati wa masomo. Pia ukosefu wa chakula huchochea sana utoro na wanafunzi kuacha shule. Utoro katika sura mbili, sura ya kwanza wanafunzi kutokuja shule na sura ya pili mwanafunzi au wanafunzi kutohudhuria kipindi au vi