BABA KAMA BABA
Baba la Baba Leo tarehe 21 June ndiyo siku ya wenye miji, watu wenye maamuzi nyumbani, watu wenye sauti popote pale ndani hata nje ya nyumba. Ni ukweli, leo ni siku ya watu ambao hawaoni shida kuvuja jasho ili wengine wafurahie leo na kesho yao. Kwa uthabiti kabisa na kuiweka familia nzima mabegani na kutembea huku kaibeba bila kujali hali ya nchi kiuchumi au iwe mvua liwe jua majukumu yake lazima atekeleze. Leo ni siku ya akina Baba Duniani, watu wenye mioyo yao. Kwa muda sasa kumekuwepo kwa siku hii adhimu ya kuhadhimisha uwepo wa akina Baba na mchango wao katika maisha na ustawi wa wanafamilia. Baba ni mzazi wa kiume, baba ni kiongozi wa familia (kwa mila za sehemu nyingi duniani). Kutokana na tamaduni na hali ya maisha ya Afrika akina baba ndiyo wamekuwa watafutaji wakubwa wa mkate wa kila siku katika familia. Kipato hicho ndiyo kitagawanywa na kutumika kama chakula, kama ada, manunuzi ya nguo za wanafamilia, nauli za hapa na pale na matumizi mengine mengi yasiyo na id