MAADHIMISHO YA SIKU YA MOYO DUNIANI
Siku ya moyo duniani huadhimishwa tarehe 29 mwezi septemba kila mwaka. Shirikisho la moyo duniani ndio chimbuko la siku hii muhimu yenye lengo la kusaidia jamii kujua madhara ya magonjwa ya mfumo wa mzunguko wa damu ambapo zaidi ya nusu ya vifo vyote vitokanavyo na magonjwa yasiyo ya kuambukiza duniani husababishwa na magonjwa haya. Hapo awali siku ya moyo duniani ilikuwa ikiadhimishwa jumapili ya mwisho ya mwezi wa tisa na kwa mara ya kwanza iliadhimishwa tarehe 24 septemba 2000. Magonjwa ya mzunguko wa damu husababisha takribani vifo vya watu milioni 17.9 dunia nzima na vifo hivi haswa huhusisha magonjwa ya moyo na kiharusi (stroke). Hii huchangia takribani asilimia 31 ya vifo vyote duniani. Moyo ni ogani ifanyayo kazi kama pampu inayosukuma damu kupitia mirija katika mwili wa binadamu na hivyo husaidia katika kusafirisha na kuzungusha virutubishi na hewa za oksijeni, kabonidayoksaidi pamoja na vitu vingine vingi. Moyo huanza kufanya kazi kuanzia siku ya 22 tangia kutung...