Posts

Showing posts from April 24, 2020

Ujinga ni kama Ugonjwa

Image
Ujinga ni kitendo cha kutokujua jambo au kitu fulani na kuathirika kwa kutokujua hilo jambo. Vivyo hivyo hata ugonjwa ni kuwa na vijidudu/vimelea mwilini na kuathirika kwa uwepo wa hivyo vimelea.  Kuna aina mbalimbali za magonjwa ila aina mbili kuu. Magonjwa ya kuambukizika na magonjwa yasiyoyakuambukizika. Ugonjwa wa kuambukizika mtu huupata kutoka kwa mwingine na kisha huuambukiza kwa wengine na mzunguzuko huendelea. Na ujinga upo katika mtindo huo. Mtu hupata maarifa asi kisha huyasambaza kwa wengine na kuwaaminisha na wale waaminio husambaza kwa wengine na wengine. Mwaka 2016 huko mkoani Dodoma wanakijiji wakishirikiana na uogonzi wa kijiji waliwaua kwa kuwachoma moto watafiti wa masuala ya ardhi. Moja ya watu wanaoheshimiwa na kuaminika pale kijijini alizusha kuwa wale wageni walioingia kwenye kile kijijini sio wataalamu kutoka kwenye taasisi bali ni wanyonya damu. Wanakijiji wakajazwa huu ujinga na wakijua wanyonya damu ni wauaji basi wakaona wawavamie...