Ujinga ni kama Ugonjwa
Ujinga ni kitendo cha kutokujua jambo au kitu fulani na kuathirika kwa kutokujua hilo jambo. Vivyo hivyo hata ugonjwa ni kuwa na vijidudu/vimelea mwilini na kuathirika kwa uwepo wa hivyo vimelea.
Kuna aina mbalimbali za magonjwa ila aina mbili kuu. Magonjwa ya kuambukizika na magonjwa yasiyoyakuambukizika. Ugonjwa wa kuambukizika mtu huupata kutoka kwa mwingine na kisha huuambukiza kwa wengine na mzunguzuko huendelea. Na ujinga upo katika mtindo huo. Mtu hupata maarifa asi kisha huyasambaza kwa wengine na kuwaaminisha na wale waaminio husambaza kwa wengine na wengine.
Mwaka 2016 huko mkoani Dodoma wanakijiji wakishirikiana na uogonzi wa kijiji waliwaua kwa kuwachoma moto watafiti wa masuala ya ardhi. Moja ya watu wanaoheshimiwa na kuaminika pale kijijini alizusha kuwa wale wageni walioingia kwenye kile kijijini sio wataalamu kutoka kwenye taasisi bali ni wanyonya damu. Wanakijiji wakajazwa huu ujinga na wakijua wanyonya damu ni wauaji basi wakaona wawavamie na kuwaua. Waliwachoma moto wale watafiti pamoja na gari yao walioenda nayo kule kijijini.
Lilikuwa tukio la kusisimua na kusikitisha sana kwa watu mbalimbali hususani kwa wasomi ambao pia maisha na kazi zao hutegemea tafiti hivyo kuona vijijini si salama.
Lakini majonzi yote haya ni zao la ujinga wa wale wanakijiji walipoambukizana kisha kugharimu maisha ya watu wengine wasio na hatia na tegemeo la taifa.
Tukiwa kipindi hivi cha janga la gonjwa la Korona. Mtu mwenye virusi vya Korona akikaa na mtu asiye na virusi anaweza akamuambukiza gonjwa hilo kwa namna mbalimbali. Korona inatesa na kuua na pia Korona inaponyeka mtu anarudi katika hali yake ya kawaida.
Ujinga ni kama ugonjwa unaambukizika, unatesa au kuua na unatibika.
Kuna mengi yasiyo ya kweli huongelewa sana kwenye jamii na watu huyaamini na baadae huyasambaza mtaa mpaka mtaa au vizazi mpaka vizazi. Hadithi za vyanzo vya vifo vya watu kwa mfano kwa sasa mtu akifa watu wanasema na kuaminishana kuwa kafa kwa Korona japo si kweli. Pia kuambukizana hadithi za vyanzo vya utajiri wa watu, sababu za matatizo ya mtu fulani, namna za kusuluhisha matatizo kwa njia za kienyeji nk na ni kwasababu hiyo watu wanajihusisha sana na ushirikina wa kuua vikongwe na maalbino kwa kuaminishana utajiri utapatikana kwa njia hiyo na si kujituma na kuwekeza. AMKA TAFUTA MAARIFA!
Njia za kupambana na ujinga wa Kuambukizika.
1. Kuwa mwepesi kuhoji au kuuliza maswali juu ya jambo unaloelezwa.
2. Tumia vyanzo mbalimbali vya kuaminika kupima ukweli wa jambo uliloambiwa. Mfano vyombo vya habari vya kuaminika, wataalamu wa jambo unaloelezwa. Inaweza ikawa Daktari, mchungaji nk
3. Kuwa mdadisi au mtafiti wa mambo. Jifunze kujithibitishia kabla ya kuamini.
4. Aliyekudanganya mara ya kwanza usimwamini haraka.
5. Jisomee na uwe na maarifa ili iwe rahisi kujua jambk la uongo na jambo la kweli kwa haraka.
AMKA TAFUTA MAARIFA
By
Nobel Edson Sichaleh
Fasmo Tanzania
0783961492
Comments