Njia 10 Nyepesi za kupata Maarifa Katika Mazingira ya Tanzania
Maarifa ni taarifa iliyobeba ukweli, ufananuzi, ujuzi, uelewa wa jumla wa kitu fulani. Kuna njia mbalimbali za kutapa maarifa. Kwa mazingira yetu ya kitanzania kuna njia nyingi za kupata maarifa na zifuatazo ni njia 10 nyepesi za kutumia katika jamii zetu.... Njia 10 za kupata maarifa ● Kujisomea vitabu mbalimbali, magazeti, makala, Majarida, vitabu vya dini. Maarifa mengi yamewekwa kwenye mfumo wa maandishi. ●Kuhudhuria semina, vikao na warsha mbalimbali. Hiyo ni pamoja na ibada za dini, Kliniki za afya, maonyesho kama vile Nanenane na mikusanyiko mingine inayohusu utoaji wa elimu. ● Simulizi, maonyo, ushauri kutoka kwa wazee na watu waliotuzunguka . Dondoo za vitu na visa mbalimbali vya kweli vya maisha hupatikana katika mfumo huu. Wazee wetu kwa uzoefu wao wa maisha na upendo wao kwetu hutuelimisha na kutupa mwongozo wa njia zipi salama katika mambo mbalimbali ya maisha. ● Kutazama Video zinazoelimisha (YouTube, Dokumentari, na vipindi vya kueli