Siku ya Maziwa Duniani. Tusherekee au Tusimame na Kujitafakari?
MAZIWA MAZIWA MAZIWA! Tulipokuwa shuleni tulijifunza makundi ya Wanyama kulingana na sifa zao. Moja ya kundi hili ni mamalia ambao sifa yao kuu ni Wanyama wanaonyonyesha akiwemo popo, binadamu, mbwa, ng’ombe, mbuzi, kondoo nk. Wanyama hawa hufanya hivi kwa kipindi Fulani na kuacha kunyonyesha mtoto/watoto wao. Kwa mfano, ndama wa ng’ombe haachishwa akiwa na umri wa miezi 4 hadi 5, baadhi ya jamii za nyani huendelea kunyonyesha watoto wao hadi wanapofikia umri wa miaka 4 wakati tembo huendelea kumnyonyesha mtoto wake hata akiwa na umri wa Zaidi ya miaka 2. Hii ina maanisha kila mnyama anaezalisha maziwa ni kwa ajili ya mtoto/watoto wake tu. Pia tutakubali kuwa kila mnyama ana tabia zake katika kumuachisha mtoto wake kunyonya. Kwa binadamu, inashauriwa mtoto anyonyeshwe hadi atakapotimiza umri wa miaka 2 na ikiwezekana aendelee kunyonyeshwa, ingawa watu wengi hawafanyi hivyo. Wengine huishia mwaka mmoja na nusu na kuacha kumnyonyesha mtoto wake. Leo ni kilele cha maadh...