USIACHE KUONGEA NA WATU
USIACHE KUONGEA NA WATU. Habari yako! Ni matumaini yangu upo salama na unachukua tahadhari stahiki katika mapambano dhidi ya Korona. Unapojizuia kupata maambukizi pia wakumbushe wengine wajizuie. Usiache kuongea nao! Viumbe hai vyote vina njia za mawasiliano. Namna ya kuwasiliana kati yao hususani pale wanapotekea familia moja. Kwa mfano Simba kwa simba, Nyani kwa Nyani, Siafu kwa siafu nk. Wakati viumbe vingine vyote vinatumia milio ya asili zao na ishara kuwasiliana baina yao binadamu yeye anatumia Lugha yaani mpangilio wa sauti kuwasiliana. Binadamu anaongea. Katika kuongea kuna... ●Kuuliza ●Kueleza/Kufafanua Katika maongezi yetu basi kuna mambo mawili tunayafanya nayo ni Kuuliza au Kueleza. Usiache kuuliza, usiache kueleza (kujieleza, kuelezea) vitu mbalimbali kwa watu waliokuzunguka. Watu wana vitu wanapitia, wana vitu wamezoea, wana vitu wanapenda jitahidi waongeleshe. Waulize ilikuwaje hivi? Wape nafasi wajieleze kuliko kuhukumu na kulaumu. Hakuna mtu mjin...