VIRUSI VYA KORONA KWA WAJAWAZITO NA WANAWAKE WANAONYONYESHA
Ugonjwa wa Coronavirus (COVID-19) ni ugonjwa unaoambukiza unaosababishwa na virusi vya corona. Virusi hivi hushambulia mfumo na hewa na kuleta madhara kadha wa kadha kwenye mwili wa mwanadamu na hata kupelekea kifo. Kumekuwa na nadharia na maswali mbalimbali juu ya virusi hivi kwa watoto wachanga, wajawazito na wanawake wanaonyonyesha juu ya namna ya uambukizaji na namna nzuri za kuzuia maambukizi. Hadi sasa hakuna utafiti unaothibitisha maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kupitia maziwa ya mama, maji maji katika mfuko wa uzazi (mtoto akiwa tumboni) au sampuli zingine kutoka kwa mama. Bado shirika la afya duniani linasema hakuna uthibitisho wa virus hai vya corona katika sampuli tajwa hapo juu. Lakini mpaka sasa kinachofahamika ni kwamba watoto kadhaa wamepatikana na virusi vya corona baada tu ya kuzaliwa na haijulikani kama walivipata wakiwa tumboni au baada ya kuzaliwa. Pia vipo visa vya mtoto wa miezi sita, miezi kumi na moja na visa ...