Posts

Showing posts with the label Poem

Shairi: IWE LEO

Image
IWE LEO Naomba iwe leo, Kesho mbona mbali? Tuwaongeze upeo, Wakulima kila mahali, Wapate maendeleo, Kwa sera za serikali. Furahisha wakaribu, Wambali watasogea, Serikali inayo sababu, Wakulima kutetea, Miaka wapata tabu, Hayupo kuwasemea. Bajetiye iwe nono, Wafikiwe vijijini, Wapanuliwe maono, Wasilime kizamani, Waachie la mkono, Wahifadhi ghalani. Jicho umwagiliaji, Sayansi shambani, Wapate mengi maji, Wasingoje mvuani, Waongeze uzalishaji, Tuwauzie majirani. Kilimo kipae thamani, Nao wakwae ukwasi, Walioko shambani, Waendelee kwa kasi, Wote wa masokoni, Uchumi wajinafasi. Miundombinu mazingira, Isiyotegemea misimu, Wapewe malengo dira, Vikundi wapate elimu, Kilimo kifanyike ajira, Kisiishie kuwakimu. Kweli kesho nayo siku, Lakini leo yawezekana, Tupitishe sera sumaku, Kilimo kiwavutie vijana, Wengi wakimbilie huku, Kilimo kiwe cha maana. Paza Sauti Wakulima Wanyanyuke Kiuchumi, Kiteknolojia na Kiuzalishaji. Imeandaliwa na, Nobel E Sichaleh. 0783961...

Shairi: IWAJE?

Image
IWAJE? Wewe ulitakaje? Shule za msingi Vitu vifanyikaje? Katikati ya vipindi Watoto walaje? Kwa elimu-ushindi Mimi kama wewe Nina uwezo kufikiri Nafikiri mwenyewe Siwezi shikiwa akili Mwenye haki apewe Vinginevyo ni ukatili Haki ya kuelimika Na malezi stahiki Hakizo kuzishika Mtoto huwa rafiki Mzaziye wajibika Utajaona mantiki Mapumziko wasile! Darasani waingie Njaa iwazingile Somo lisiwaingie Shule waikimbie Maoniyo niambie? Wale chakula vizuri Darasa changamfu Wasipate tena sifuri Utoro ugeuke hafifu Wawe watoto wazuri Wenye afya nadhifu. Changia mawazo Tupate mwongozo Tuwajengee uwezo Elimu bora ni nguzo Hatua hizi mwanzo Tuvishinde vikwazo #NilisheNifaulu Fasmo Tanzania Nobel was Here😊

Shairi: BINTI MTOTO WA KIKE

Image
Poem Leo ndio ile siku yao, Mabinti kusherekea, Waongee vitu vyao, Yatupasa vipokea, Magumu waseme wao, Yawapasa kuendelea. Binti Mtoto wa kike,  Amka kwa pambazuka, Yenye tija uyashike, Wakati wako umefika, Kimaendeleo utumike Wasiokuamini kuaibika. Punguza kupiga soga, Na umbea kila kukicha,  Wahabarishe mashoga, Waamke kumekucha, Waachane na uoga, Maendeleo kujiepusha Kujituma iwe tabia, Usingoje uhimizwe, Jamii inakusubiria, Ndoto zako utimize, Yasokufaa kimbia, Usisubiri yakuumize. Mimba kabla ya ndoa, Rafiki hilo usithubutu, Kimaisha litakupopoa, Na kushusha wako utu, Haswa akikataa kukuoa, Ndoto zako tapata kutu. Wewe mtu adhimu, Acha leo nikupashe, Ndoto zako muhimu, Usikubali usiziache, Ongeza na nidhamu, Sibwetekee uchache. AMIN Na  Nobel Edson  Fasmo Tanzania 0783961492

Shairi: TUISHINDE CHUKI

Image
Tuishinde Chuki Nasaha lukuki, Leo tusemezane, Tuishinde chuki, Mbinu tupeane, Isilete taharuki, Mwisho tuuane. Chuki roho chafu, Hasara abadani, Watu waliodhaifu, Huitunza kifuani, Tabia ya siafu,  Kujitia hatiani. Chuki mitaani, Imefika bungeni, Imeingia kanisani, Upendo pembeni, Tupendane jamani, Itasaidia mbeleni. Alimchukia Sadiki, Akapanga mpoteza, Kumvamia alidiriki, Ghafla akateleza, Akapoteza umiliki, Sasa magereza. Chuki huleta aibu, Hilo jambo jua, Waumbuka kiajabu, Waangukia pua, Utaishi kwa taabu, Utawaza jiua. Ndugu twachukiana, Sisi kwa sisi, Kutwa twawindana, Twaishi kifisi, Twashindwa samehana, Tumejawa ubinafsi. Samehe mara sabini, Na ukiweza sahau, Zinashauri dini, Kumbuka hilo mdau, Tukirudi vumbini, Upendo utawale walau. Tusamehane ndugu, Chuki ndani ondoa, Yaweza geuka rungu, Kisha uhai ikakutoa, Haimpendezi Mungu, Hakika yatutia doa. Na Nobel Edson Sichaleh Fasmo Tanzania

SHAIRI: NJIA PANDA

Image
NJIA PANDA Nipo njia panda, Mawazo yanizonga, Kiza kimetanda, Fikra zanigonga, Wapi pa kwenda, Kivipi nitasonga? Niache shule, Nikatumie kipaji, Niwe kama yule, Msanii mchezaji, Nivume huku kule, Kwa mdogo mtaji. Nitakuwa maarufu, Na hela kibao, Sitaishi kwa hofu, Yatakuwaje mafao, Hawatoacha kunisifu, Katika maongezi yao. Nitajenga majumba, Nakumiliki magari, Kupitia kuimba, Nitakuwa hodari, Kwa udi uvumba, Nitaiteka sayari. Shule kitu nyeti, Lakini mimi sielewi, Kwanini wenye vyeti, Nafasi hawapewi, Kwenye viti waketi, Haki hawatendewi. Shule haina manufaa, Wasomi maisha duni, Sasa wanatuhadaa, Kisiasa kuturubuni, Kutuaminisha wanafaa, Wajinufaishe kiuchumi. Kipaji changamoto, Nani wa kukusaidia, Utaishia kwenye msoto, Na kuchoka kuvumilia, Utalia kama mtoto, Ndoto zisipotimia. Elimu bado hazina, Kote ulimwenguni, Kuiacha hapana, Hata wakinirubuni, Nitakosa maana, Wataniita muhuni. Shairi la watoto..... Na Nobel Edson Sichaleh Fasmo Tanzania  Childhood Develop...

MAZIWA KAMA MAZIWA (Shairi)

Image
MAZIWA KAMA MAZIWA Maziwa yamejaa lishe, Kuchochea afya nzuri, Ngoja leo nikuelimishe, Hili jambo la maakuli, Faida nizibainishe, Unywaji uwe vizuri. Kinywaji burudishi, Hakika afya chafaa, Kimejaa virutubishi, Na madini kadhaa, Kiweke kwenye pishi, Chakula kitamu balaa. Kimejaa protini, Wanga jitosheleza, Utashiba vitamini, Maji mwilini utaongeza, Mafuta na madini, Maziwa sio yakubeza. Mifupa huimarika, Kinga huongezeka, Hutoweza kutaabika, Mbeleni ukizeeka, Yafaa kwa kila rika, Na mwili hutosheka Ya ng'ombe au mbuzi, Kunywa kila mida, Wanashauri wajuzi, Mwilini hutopata shida, Changanya na mchuzi,  Mwili upate faida. Mwambie na jirani, Elimu hii imfikie, Maziwa si utani, Kunywa asipuuzie, Akisema ni uzamani, Faida zake msisitizie. Na  Nobel Edson Sichaleh, Fsmo Tanzania. Nutritionist and Consumer Scientist 0783961492

Shairi: LISHE NAISHIKIA KIPAZA

Image
LISHE NAISHIKIA KIPAZA Leo jukwaani najongea, Sauti yangu kuipaza, Kuna kitu nataka kuongea, Muda sasa cha nikwaza, Wasio na sauti wataponea, Rafiki yao nashika kipaza. Ni kwa muda sasa, Jamii yetu ii taabani, Lishe yaonekana anasa, Wakulaumiwa nani? Viongozi wa kisiasa, Au mitaala ya kizamani? Tunazalisha mazao, Hatujui kuyatumia, Watu wala kikwao, Vyakula hufakamia, Shida huja afya zao, Gharama kujitibia. Laiti ingetolewa elimu, Mitaani na darasani, Wangejua umuhimu, Nini kiwepo kwa sahani, Magonjwa wangekuwa adimu, Ukosefu wa vyakula fulani. Bungeni ingekuwepo kamati, Yenye uongozi makini, Iliyojaa mipango mikakati, Kuwafikia watu wa chini, Na kuwawezesha kwa dhati, Elimu ya lishe waushinde umaskini. Lishe kwa mtoto na mama, Ila sio kwa wao tu aisee, Lishe ni jambo la maana, Kwa vijana pia wazee, Wote tuseme hapana, Kula mlo mmoja pekee. Mkulima ukitoka kuvuna, Mavuno hifadhi vizuri, Pindi yatapokuwa hakuna, Ghala lako lisiwe sifuri, Utaendelea kutafuna, Ukifanya zingine shughuli. K...