MAZIWA KAMA MAZIWA (Shairi)

MAZIWA KAMA MAZIWA
Maziwa yamejaa lishe,
Kuchochea afya nzuri,
Ngoja leo nikuelimishe,
Hili jambo la maakuli,
Faida nizibainishe,
Unywaji uwe vizuri.

Kinywaji burudishi,
Hakika afya chafaa,
Kimejaa virutubishi,
Na madini kadhaa,
Kiweke kwenye pishi,
Chakula kitamu balaa.

Kimejaa protini,
Wanga jitosheleza,
Utashiba vitamini,
Maji mwilini utaongeza,
Mafuta na madini,
Maziwa sio yakubeza.

Mifupa huimarika,
Kinga huongezeka,
Hutoweza kutaabika,
Mbeleni ukizeeka,
Yafaa kwa kila rika,
Na mwili hutosheka

Ya ng'ombe au mbuzi,
Kunywa kila mida,
Wanashauri wajuzi,
Mwilini hutopata shida,
Changanya na mchuzi,
 Mwili upate faida.

Mwambie na jirani,
Elimu hii imfikie,
Maziwa si utani,
Kunywa asipuuzie,
Akisema ni uzamani,
Faida zake msisitizie.
Na 
Nobel Edson Sichaleh,
Fsmo Tanzania.
Nutritionist and Consumer Scientist
0783961492


Comments

Popular posts from this blog

Mitindo Yetu Ya Ulaji.

Nafasi ya Maziwa katika Afya Zetu.

MADHARA YA UTENGANO WA KIJAMII YALIYOSABABISHWA NA COVID19