Posts

Showing posts from July 13, 2020

Mpango Binafsi wa Afya.

Image
Tanzania ni moja ya nchi zilizopo kusini mwa jangwa la sahara zenye idadi kubwa ya watu. Licha ya serikali ya Tanzania kufanya jitihada nyingi katika kupambana na maadui watatu ambao ni Ujinga, umasikini na Maradhi bado kuna changamoto kubwa kwenye jamii za Kitanzania hususani kwenye afya na lishe. Watu wengi bado hawana elimu toshelezi juu ya ulaji bora na mitindo mizuri ya maisha itakayowaepusha na matatizo ya kiafya na kilishe. Idadi kubwa ya Watanzania bado ina jikongoja katika kukamilisha milo mitatu kwa siku. Huku idadi kubwa zaidi ikiwa bado gizani katika kupangilia makundi ya vyakula katika mlo. Yote haya yanasababishwa na ukosefu wa elimu ya lishe kwa sehemu kubwa na pia umasikini unachangia kwa sehemu hali kuwa mbaya zaidi. Kwa kuwa wapo wenye uwezo wa kula watakavyo (idadi kubwa ya milo) lakini bado hawaipangilii vizuri. Changamoto nyingine iliyopo kwenye afya na lishe kwa Watanzania wengi ni ukosefu wa tamaduni au tabia ya kuzingatia kanuni za mambo mbalimbali. Maisha yetu ...