Shairi: BINTI MTOTO WA KIKE
Poem Leo ndio ile siku yao, Mabinti kusherekea, Waongee vitu vyao, Yatupasa vipokea, Magumu waseme wao, Yawapasa kuendelea. Binti Mtoto wa kike, Amka kwa pambazuka, Yenye tija uyashike, Wakati wako umefika, Kimaendeleo utumike Wasiokuamini kuaibika. Punguza kupiga soga, Na umbea kila kukicha, Wahabarishe mashoga, Waamke kumekucha, Waachane na uoga, Maendeleo kujiepusha Kujituma iwe tabia, Usingoje uhimizwe, Jamii inakusubiria, Ndoto zako utimize, Yasokufaa kimbia, Usisubiri yakuumize. Mimba kabla ya ndoa, Rafiki hilo usithubutu, Kimaisha litakupopoa, Na kushusha wako utu, Haswa akikataa kukuoa, Ndoto zako tapata kutu. Wewe mtu adhimu, Acha leo nikupashe, Ndoto zako muhimu, Usikubali usiziache, Ongeza na nidhamu, Sibwetekee uchache. AMIN Na Nobel Edson Fasmo Tanzania 0783961492