Posts

Showing posts from April 15, 2020

Ujinga Humfanya Mtu aishi kwa Kujibalaguza

Image
Kuna madhara mengi ya ujinga kwa mtu. Mtu akiwa na ujinga hujikuta akitegemea watu wengine ili afanikiwe kwenye anachotaka kutokana na kushindwa kufuzu vigezo vya taaluma, ujuzi na maarifa ambavyo vingemfanya apate hicho cheo, kazi au nafasi. Mtu mjinga kwa kukosa sifa stahiki hujikuta akijikomba kwa wenye uwezo wa kumsaidia apate anachohitaji. Hii hali huondoa hata heshima yake kwa jamii na hata kumfanya yeye kufanya vitu vya ajabu ili tu alipwe fadhira au alipe fadhira. Pia ujinga wa kutojua thamani yako, kutoheshimu hali yako au kipato chako na haki zako utapelekea mtu kujibalaguza kwa watu wengine ili uonekane upo kama wao au upate vitu fulani. Tafuta maarifa, jifunze kujitegemea.... Amini katika uwezo wako.... pangilia mipango yako. Fanya kwa juhudi. 

Ujinga Humfanya Mtu Asistaarabike!

Image
Ukosefu wa maarifa humpelekea mtu kukosa ustaarabu unaohitajika katika jamii au ustaarabu unaotarajiwa binadamu auonyeshe. Na sio tu mtu hushindwa kustaarabika akiwa mbele ya wanajamii lakini pia akiwa peke yake. Tabia zinazoweza kukwaza watu wengine au kuleta athari kwake na kwa jamii. Mfano mwepesi uvutaji wa sigara hadharani au hata kwenye maficho. AMKA TAFUTA MAARIFA #ATM2020 #againstignorance #againstviolence

Àmka Tafuta Maarifa

Image
Kwa kutokujua umuhimu wa kile unachokifanya ikitokea changamoto yoyote unajikuta unakuwa mwepesi kukata tamaa kuendelea kufanya kile kitu ambacho kingekuletea faida huko mbeleni. Kuna watu waliacha shule bila sababu ya msingi, kuna watu wametelekeza familia na wanapoulizwa kwanini hawaishi kujitetea.  Moja ya madhara ya ujinga ni kukata tamaa haraka, ukijua thamani ya kazi au ndoto yako hutoikatia tamaa haraka mpaka uyaone matunda yake. Je nini unahitaji maishani? AMKA TAFUTA MAARIFA juu ya kile unachokitaka kijue nje ndani kisha wekeza juhudi na ubunifu utafanikiwa.  #ATM2020  #educateyourself #kitaaolojia #againstignorance  #hardworkpaysoffs