Ujinga Humfanya Mtu aishi kwa Kujibalaguza

Kuna madhara mengi ya ujinga kwa mtu. Mtu akiwa na ujinga hujikuta akitegemea watu wengine ili afanikiwe kwenye anachotaka kutokana na kushindwa kufuzu vigezo vya taaluma, ujuzi na maarifa ambavyo vingemfanya apate hicho cheo, kazi au nafasi. Mtu mjinga kwa kukosa sifa stahiki hujikuta akijikomba kwa wenye uwezo wa kumsaidia apate anachohitaji. Hii hali huondoa hata heshima yake kwa jamii na hata kumfanya yeye kufanya vitu vya ajabu ili tu alipwe fadhira au alipe fadhira.

Pia ujinga wa kutojua thamani yako, kutoheshimu hali yako au kipato chako na haki zako utapelekea mtu kujibalaguza kwa watu wengine ili uonekane upo kama wao au upate vitu fulani.
Tafuta maarifa, jifunze kujitegemea.... Amini katika uwezo wako.... pangilia mipango yako. Fanya kwa juhudi. 


Comments

Popular posts from this blog

Mitindo Yetu Ya Ulaji.

Nafasi ya Maziwa katika Afya Zetu.

MADHARA YA UTENGANO WA KIJAMII YALIYOSABABISHWA NA COVID19