Àmka Tafuta Maarifa

Kwa kutokujua umuhimu wa kile unachokifanya ikitokea changamoto yoyote unajikuta unakuwa mwepesi kukata tamaa kuendelea kufanya kile kitu ambacho kingekuletea faida huko mbeleni. Kuna watu waliacha shule bila sababu ya msingi, kuna watu wametelekeza familia na wanapoulizwa kwanini hawaishi kujitetea. 
Moja ya madhara ya ujinga ni kukata tamaa haraka, ukijua thamani ya kazi au ndoto yako hutoikatia tamaa haraka mpaka uyaone matunda yake. Je nini unahitaji maishani? AMKA TAFUTA MAARIFA juu ya kile unachokitaka kijue nje ndani kisha wekeza juhudi na ubunifu utafanikiwa. 
#ATM2020  #educateyourself #kitaaolojia
#againstignorance  #hardworkpaysoffs

Comments

Popular posts from this blog

Mitindo Yetu Ya Ulaji.

Nafasi ya Maziwa katika Afya Zetu.

MADHARA YA UTENGANO WA KIJAMII YALIYOSABABISHWA NA COVID19